ANGALIA PICHA DAKTARI FEKI AKAMATWA MUHIMBILI
Hospitali
ya taifa ya Muhimbili imemkamata mtu mmoja anae sadikiwa kuwa daktari
feki ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akitapeli wagonjwa wanaoenda
kutibiwa katika hospitali hiyo ya taifa kwa namna mbalimbali Daktari
huyo aliyejulikana kwa jina la Kitano Mustafa Kitani mwenye umri miaka
51 anadaiwa kuwa alikuwa anajitambulisha kama daktari upande wa akina mama katika hospitali ya Muhimbili.
Hospitali
ya taifa ya Muhimbili mbali na utaratibu wa kutumia vitambulisho kwa
wafanyakazi ili kuondoa tatizo kama hili, bado tatizo hili limeendelea
kujitokeza
Hospitali
ya Muhimbili inawataka wafanyakazi wake wanaoshirikiana na madaktari
vishoka kuacha tabia hiyo yenye athari kwa wagonjwa na taifa.
Chama cha Madaktari nchini kimewataka wananchi kuwa macho na madaktari wanaojitokeza kutaka kusaidia wagonjwa.
Wakati daktari huyo akidai yeye ni
daktari kitaaluma, Afisa Usalama hakubaliani nae kutokana na taarifa za
kiuchunguzi kuthibitisha kuwa ni feki.
Hili ni tukio la tatu kutokea katika hospitali ya Muhimbili
Comments
Post a Comment