ANGALIA PICHA AUNGUZWA NA MAFUTA YA MOTO KISA VOCHA

MKASA MZIMA ULIKUWA HIVI.....

Kijana mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mke wa mtu anateseka hospitalini baada ya kuchomwa na mafuta ya kupikia ya moto na ndugu yake baada ya kuhisiwa kuiba vocha ya simu ya mtandao wa Telecel yenye thaman ya senti 50 huko Zimbabwe.Kijana huyo aliyejulikana kwa jina la Otilia Kosa anayeishi Plot 16, Tsungwizi Ridge maeneo ya Nyazura huko nchini Zimbabwe anateseka katika hospitali ya Rusape General Hospital akiuguza majeraha aliyoyapata baada ya kumwagiwa mafuta ya moto na ndugu yake.

Inadaiwa kwamba mnamo tarehe 27 Decemba 2013, Otilia alimuuliza ndugu yake Kudakwashe kama yeye ndiye aliyetumia vocha yake ya mtandao wa Telecel yenye thamani ya senti 50 za kizimbabwe.Kudakwashe alikataa kuwa hakutumia vocha hiyo na hapo ndipo mtafaruku mkubwa ulipotokea kati ya wawili hao.
Cha kushangaza ,siku iliyofuata kikao cha familia kilikaa ili kuwapatanisha wawili hao ambao walishindwa kuelewana na mpaka kufikia hatua mbaya ambayo ingepelekea kuvunja udugu wao.Hata hivyo, wanafamilia hao walishindwa kuwapatanisha ndugu hao na hivyo kuongeza mpasuko kati yao.
Ilidaiwa kuwa baada ya kukosa muafaka huo,Kudakwashe alipatwa na hasira kali iliyompelekea yeye kuingia jikoni na kuchemsha mafuta ya kupikia na kummwagia nduguye huyo (Otilia) katika maeneo ya uso,shingo,kifua,mikono na tumboni.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Afisa wa Polisi wa ZRP Nyazura, Inspekta hikima Sanida alinukuliwa akisema "We have arrested the suspect and recorded a warned and cautioned statement in which she admitted scalding the victim with hot cooking oil. She was charged with first-degree
assault and criminal violation of the Domestic Violence Act,"
Pia Inspector Sanida aliongeza kuwa kesi ilishafunguliwa Alhamisi iliyopita,lakini kesi hiyo imeahirishwa mpaka Alhamisi ijayo ambapo madaktari wamethibitisha kuwa muathirika anaweza kuhudhuria mahakamani kutoa ushahidi.

Comments

Popular posts from this blog