''USILIE KWA SABABU NITAKUFA, LIA KWA SABABU MWANAUME MWENZAKO AMENITENDA,


Nilipoingia katika mahusiano naye
nilimuamini, nikampa kila kitu
nilichoweza. Nakumbuka enzi zile
nyumbani tulikuwa tuna ng’ombe, niliiba maziwa kila siku na kumpelekea kwao.
Akanenepa!!

Penzi letu likawa huru alipoanza maisha
yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote
kuhusu mapenzi.


Alinifundisha.
Nikaegemeza maisha yangu yote kwake.Akanifany a nikawa mtumwa wa
ngono kila nikienda chumbani kwake.
Kama haikutosha sasa akaanza
kunifundisha kunywa pombe. Niliamini
kuwa ndiye mume wangu mtarajiwa,
kwa nini nikatae?

Nilimkubalia kila kitu. Alinilazimisha ngono hata nilipokuwa
katika siku zangu. Kweli nilikuwa
msomi na niliyajua madhara ya kufanya
hivyo lakini sikutaka kumuudhi huyo
niliyeamini kuwa ni mume wangu.
Nilipenda tututmie kinga lakini aliipinga sana. Nikapata mimba ya kwanza!!
Hakuwa na pesa lakini alinilazimisha
niitoe. Nikaiba pesa nyumbani
nikafanyaalivyo taka. Kwa mara ya
kwanza nika toa mimba.
Haikuniuma sana!! Niliamini kuwa ni yeye atakuja kunioa na atanifichia aibu hii.

Nilitegemea sasa tutaanza kutumia
kinga. Lakini hapana haikuwa hivyo.
Aliendelea kunilaghai. Tayari aliujua
udhaifu wangu. Alinishika hapa na pale.
Nikishtuka tayari amefanya anavyojua. Pombe kidogo na nyingine kidogo.
Nikazoea lakini nikawa na wahi kulewa.
Akautumia udhaifu huu kunifanyia jambo
baya lililonifanya niandike haya kwako.

Akaniingilia kinyume na maumbile.
Alinilawiti!! Nilishindwa kumshtaki popote.
Nikavumilia kwa kuwa alikuwa mume
wangu mtarajiwa. Mume asiyejulikana
hata kwa wazazi.
Mchezo ule ukaendelea. Akajitetea eti
hataki nipate mimba tena, hivyo hiyo ni mbinu mbadala.

Najuta kumuamini!!
Lakini huyo alikuwa mume wangu.
Miaka ikapita, ule urembo wangu
niliozoea kuuona katika kioo ukatoweka,
simu za mara kwa mara kutoka kwake
zikatoweka, akawa mkali sana kwangu. Hakutaka niende kwake. Wakati huo
nilikuwa nasoma chuo.
Pesa ya mkopo ikitoka ananitafuta na
tunakuwa marafiki tena. Anasema
ananipenda na atanioa. Ananilewesha na
kunitumia kinyume na maumbile. Pesa ikiisha na mapenzi yanaisha
nabaki mwenyewe katika msoto. Sasa
akaanza kubadilisha wasichana waziwazi.
Ningesema nini mimi?

Ninajua alishindwa kusema neno moja
tu. Tuachane!! Nilijua tayari ameniacha!!!
Afya yangu ikadolola sana,
nikalazimika kwenda kupima hospitali.
Sikuwa na virusi. Nikapewa ushauri
nikautumia.
Siku zikasonga nikampata mwanaume mwingine. Huyu alikuwa ananijali sana.
Nikaanza kumsahau yule aliyenitenda.
Nilipomaliza chuo akajitambulisha
nyumbani na alitaka kunioa.

Akanioa kweli. Maisha yakaanza. Mwaka
wa kwanza, mwaka wa pili na hadi wa tatu. Sikuwa nabeba mimba.
Mume wangu alikuwa mvumilivu sana,
hakuwahi kunilaumu. Lakini niliumizwa
na mawifi. Nikaamua kwenda hospitali.
Nikaambiwa kizazi changu kiliharibiwa
kwa kutoa mimba mara kwa mara. Pia mapenzi ya kinyume na maumbile
yamenivuruga kabisa.

Nililia sana huku nikimkumbuka yule
aliyeuleta uchungu huu kwangu.
Dunia haikuwa mahali pangu sahihi.
Nimekuandikia barua hii mdogo wangu.Uisome mwenyewe!! Lakini
uwasimulie wengi baada ya kifo changu.
Uwasimulie bila kuchoka wasichana wa
kileo wanaodanganyika na kufanya
mambo magumu kuwaridhisha wapenzi
wao. Waambie watakufa kwa mateso kama mimi.
Wasipokusikiliz a usijisikie vibaya maana
hata mimi nilikuwa siwasikilizi watu
waliponambia lolote kuhusu yule
mume mdanganyifu .
Sitajiua lakini nitakufa kabla ya wakati!!!
Nimekuandikia wewe kwa kuwa u
mwandishi. Japo kwa sasa u mtoto
mdogo najua utaipata nafasi siku moja
ya kuwafikishia wasichana hawa.
Usilie kwa sababu nitakufa. Lia
kwasababu mwanaume mwenzako AMENITENDA HIVI!!! TAFADHARI TAFAKARI''

Comments

Popular posts from this blog