NYOKA MKUBWA AINA YA COBRA AILAZIMISHA NDEGE KUTUA BILA KUFIKA MWISHO WA SAFARI

 NewsImages/6694982.jpg
NYOKA aina ya Cobra amesababisha kizaza kwenye ndege na kuilazimisha kukatisha safari yake na kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Hurghada nchini Misri, auliwa baada ya kumjeruhi abiria .Nyoka huyo alizua mtafaruku huo baada ya kutoka katika mfuko alipokuwa amehifadhiwa na kumjeruhi abiria mmoja raia wa Jordan aliekuwa amekaa karibu na mfuko uliokuwa amehifadhiwa nyoka huyo.

Abiria walianza kumshambulia wakijaribu kumuua kwa kumpiga na viatu na hatimae kufanikiwa kumuua, abiria aliejeruhiwa alipatiwa huduma ya kwanza, na kuhamishiwa hospitalini kwa matibabu zaidi na kuwekwa chini ya uangalizi kwa masaa 24, hali iliopekea kukatisha safari yake.

Uchunguzi wa awali uliofanywa umebaini kwamba, mmoja wa abiria alimficha nyoka huyo kwenye mkoba na alifanikiwa kupita katika vizuizi na kuingia na nyoka huyo kwenye ndege.

Comments

Popular posts from this blog