NEEMA KWA WANAMTWARA WASHUSHIWA UMEME HADI SH27,000
Serikali
imetangaza neema kwa vijiji vinavyopitiwa na bomba la gesi ambavyo vipo
mkoani Mtwara na Lindi, sasa wataunganishiwa kwa Sh27,000.
Hatua
hiyo ilitangazwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye uzinduzi mradi wa
umeme wilayani Nanyumbu na Masasi.
Profesa Muhongo alisema gharama za kuunganisha umeme kwa sasa ni Sh177,000.
Alisema zaidi ya vijiji 50 vimepewa upendeleo huo ili kuwawezesha wananchi kuwa na maisha bora.
Lengo la
Serikali ni kufikia asilimia 30 ya wasasatu waliounganishwa na umeme na
kwamba, hivi sasa ni asilimia 23 pekee wanaopata umeme nchini wakati
Mtwara ni asilimia nne.
Kuhusu
umeme wa gesi, Profesa Muhongo alisema Mtwara wanatarajia kuzalisha
megawati 600 ambazo baada ya matumizi nchini, zitauzwa nchi za Malawi,
Zambia na Msumbiji
Awali,
akizungumza na mamia ya wakazi wa Mangaka waliofika kushuhudia uzinduzi
huo, Pinda alisema mradi huo ni utekelezaji wa azma ya Serikali
kuhakikisha kila wilaya inapata umeme.
"Mpango
wa kupeleka umeme nchini ni wa miaka mitatu na katika sekta ya nishati
chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa ya Sasa (BRN), tumeazimia kwenda kwa
awamu," alisema.
ili
tuwafikie wananchi wengi zaidi kutoka asilimia 24 ya sasa hadi kufikia
asilimia 30 ya watumiaji wa umeme," alisema Waziri Mkuu. Chanzo:
mwananchi
Comments
Post a Comment