NAOMBA WAANDISHI WAANDIKE HABARI ZA UHAKIKA,

 TANGU SAJUKI AFARIKI NAZUSHIWA NIMEOLEWA Muigizaji wa kike wa filamu za kiswahili, Wastara Juma amesema tangu mme wake Juma Kilowoko aka Sajuki afariki anakutana na changamoto nyingi kwenye mazingira yaliyomzunguka kwa sasa.

Akizungumza na tovuti ya Times FM 100.5, Wastara amesema tangu Sajuki afariki kumekuwa na taarifa zisizo za kweli zinazodai kwamba amepata mume.
“Nina changamoto nyingi sana,unajua siku zote kama mtu ukitaka kuheshimiwa basi heshima ndio msingi wa maisha,lakini tangu mume wangu afariki (Sajuki)kumekuwa na maneno mengi sana kwenye magazeti,mara nimeolewa sijui nimevishwa pete na ukija kuangalia mtu aliyeandikia hiyo habari unamjua na ukimpigia simu anaanza kukukwepa. Kama habari za kuolewa siwezi kwanza kutangaza, naomba waandishi waandike habari za uhakika ili ujumbe ufike mzuri kwa wananchi wanaotutazama sisi Wasanii.” Amesema Wastara.

Katika hatua nyingine Wastara amesema mwaka huu amejipanga vizuri katika kutoa filamu zake mpya sinazotarajia kutoka hivi karibuni.

“Mwaka jana mwishoni nilijikita sana kwenye kuandaa filamu mpya za kwangu na nyingine nimeshiriki kwa hiyo mashabiki wakae tayari.”
CREDIT : TIMES FM WEBSITE

Comments

Popular posts from this blog