MEYA WA BUKOBA AJIUZULU RASMI LEO BAADA YA RIPOTI YA CAG KUMBANA,SOMA RIPOTI HIYO HAPA




Viongozi wote wako ukumbini,mbunge namuona mh mshashu,madiwani wote wapo.ukumbi umejaa,dc antangaza kwamba wananchi wake njee ni mkutano wa ndani,wanakubali,kwamba wasipige kelele,napata taarifa kwamba polisi wako nje wanalanda landa
viongozi wanaingia,muda wowote watasoma,tusikilize
Wabunge wanajitrambulisha na ras anatoa taarifa hii.
RAS kagera mnambila, anawakaribisha naibu TAMISEMI Mwanry na mkaguzi mwenyewe utoh wako mbele.
Ansema ni maelekezo ya waziri mkuu kufanya ukaguzi maalum na kupokea maelekezo yta serikali juu ya uakaguzi huo.
Walioalikwa-kutoka manispaa ya bukoba na wabunge
Mwanry anamwakilisha waziri mkuu, Utouh ameambatana na Bw Mero, Bi Mwadawa, Bw Nkinja, Bw Sabuni ambao wameshiriki kufanya ukaguzi bukoba mjini,hii ni taarifa inatolewa na mmoja wa maafisa,Bw rweyemamu ndiye anatoa taarifa hii.
RC anamkaribisha Utoh kuongea



Taarifa ya Utoh
Waziri mkuu alituomba tufanye ukaguzi maalum,
Mwaka 2013 tulifika bukoba na kufanya kikao cha kwanza na wadau.
Katika kikao hicho nilitoa maombi ambayo mliyafuata nawashukuru,madiwani na wananchi walitusaidia saana.

Natoa taadhari kwamba tulikuwa na baadhi za rejea ambazo ndizo tulizofuata,tulipokea maombi ya wananchi wengi lakini hayakuwepo katika rejea,hatukuyafanyia kazi
Kilichobainika
Tunapohitaji maendeleo,tunafanya vitu kwa nia njema bila kufuata taratibu
Kuhusu uwekezaji wenye mashaka kwenye kituo cha kuosha magari,zabuni haikuwa shindanishi
ni kiyume na taratibu cha taribu anataja kifungu kilichokiukwa
Waliosaini ni Khamis kaputa na anatory amani huku wakijua ilikuwa ni makosa kufanya hivyo bila idhini ya kikao cha madiwani,pia kampuni husika ya ASEC ilikuwa haijasajiliwa na BRELA. hailipi kodi TRA
2.Issue ya Viwanja
kati ya wananchi 800 waliotakiwa kugawiwa viwanja ni 300 waliogawawia kutokana na migogoro ya viwanja kimila.
Manispaa ilingia makubaliano na UTT kupima viwanja elfu 5 kwa kugawana faida ya asilimia 50 kwa 50 baina ya UTT manispaa ilisainiwa na kaimu meya ngalinda bila kupata idhini ya baraza la madiwani
Pia walikopa fedha kutoka UTT bila kupata ridhaa ya waziri mwenye thamana.
3.Issue ya matengenzo ya barabara mpya
Manispaa ya bukoba iliingia mkataba na mkandarsai aitwaye KAJUNA INVESTMENT mkataba ulikuwa wa sh 138 milioni alilipwa fedha za dharula ambazo hazikuwa na nyaraka hivyo malipo ya mkandarasi huyu yaliongezwa hadi kufikia sh sh 227 kwa kutumia barua iliyosainwa na tofauti na hali ya awali.haikuwapa idhini ya mkandarasi wa serikali na kinyume na kanuni za manunuzi ya umma.anasoma kifungu kilichokiukwa
4.issue ya Ujenzi wa soku kuu
Utaratibu wa kutaka kujenga soko kuu la bukoba haikupata idhini ya madiwani ya kumlipa mkandarasi mshauri OGM milioni 789 huku pia akawaita madiwani na kuwaeleza kuwa mkandarasi anahitaji jumla la miliini 590 milioni. Mmojawapo wa madiwani mh lunagisa alikataa pale pale kwenye kikao.
5.Issue ya kuhamisha wafanyabisha wa bukoba
Mh Meya anatory aman aliomba mkopo kwa kazi hiyo bila kibali cha madiwani na mawaziri.mkopo huo hata hivyo haukupatika
6.Mkandaasi wa OGM hakuwa kwenye orodha ya walioomba zabuni ya kufanya kazi ya ukandarasi ushauri wa kufanya kazi katika ujenzi wa soko kuu lakini alionekana kwenye rodha baadaye ya waliolipwa .Wakandarasi wote waliolipwa fedha hizo walikuwa hawalipi kodi TRA-hivyo TRA ina haki ya kuwadai hizo kodi.
7.Ujenzi wa stendi kuu ya bukoba
Mradi huu hakutengezwa kwenye gazeti la serikali lakini walipata mkandarasi na kumlipa fedha za kazi hiyo kinyume na taratibu za serikali.gazeti lilotangaza tenda hiyo halikupatikana.pia timu ya ukaguzi ilitembelea eneo la kazi na kubaini kuwa mkandarasi alilipwa fedha nyingi tofauti na kazi aliyoifanya
9.Mradi wa maji
Kila kata iliyopangwa kuwekwa mradi wa maji ilitakiwa kuchangia asilimia 2 hivyo kata anakotoka meya ilitimiza kigezo na kupata huduma hiyo.fedha za kata zilitolewa na meya kwa kata yake.hivyo kitendo cha kata ya meya kupata huduma hakuwa na tatizo.Tuhuma hizi kuwa meya alitoa huduma kwa kata yake ni uongo.
10.Issue ya uuzwaji viwanja vya wazi.
Mkataba wa kununua kiwanja kinacholalamikiwa hakufuata taratibu za ununuzi
Ni katika bweni la sekondari ya PEACE inayomilikiwa na Meya.Tunapendekeza kuundwa kwa timu maalumu kuchunguza tuhuma hizi kwani katika eneo hili hatukufikia mwisho
11.Ujenzi wa barabara kwa lami kwenye kata ya meya toafuti na fedha zilizoombwa
Manispaa iliomba milioni 30 kukarabati barabara hiyo lakini TAMISEMI ilitoa milioni 300 na walihoji TAMISEMI walisema hilo ni la kawaida hivyo tuhuma hizo ni UONGO
12.Mradi wa Ujenzi wa Bwawa 
Hakuwahi kujadiliwa na baraza la madiwani,ulikuwa ni mradi wa wajanja tu
13.Issue ya wafanyabishara soko kuu kutolipa kodi
Manispaa Imekosa mapato sh milioni 256 zimepotea kutokana na chanzo hicho cha wafanyabishara wa soko kuu kutolipa kodi kutokana na mgogoro unaondelea
14.Issue ya matumizi ya gari Sm 4663
Gari hili limekuwa likiegeshwa kwa ofisi ya redio kasibante ya kagasheki.kumbukumbu za TRA zinaonesha kuwa ni mali ya halmashauri lakini alipohojiwa kagasheki alidai kuwa alinunua kwa fedha zake. Lakini halmashauri haina kumbukumbu zozote juu ya gari hilo
Tunapendekeza lilerejeshwe kwenye halmshauri kama ataona ni manufaa kwa wananchi lakini kama haitawezekana basi gari hilo libadilishiwe usajili ili lionekane ni la kiraia
15.Uteuzi wa wakala wenye upendeleo kwenye ushuru wa basi
Zabuni ya aliyepata rufaa ilitenguliwa kwani haikuwa imesajiliwa na mamlaka husika
Alibadilisha jina na kuomba tena kisha kupata,muombaji aliyeomba kwa tozo ya juu alinyimwa.
Manispaa ilifanya upendeleo na kukosa sh million 46 kwa mwaka
16:Issue ya posho kwa madiwani katika safari ya mafunzo nje ya wilaya.
Madiwani wawili walitakiwa kulipwa sh laki 4 kila mmoja kwa safari hawakusafiri lakini fedha hizo hazikurudishwa kwa manispaa na kukatiwa risiti,.hazionekani zilipo
17.Issue ya vibanda vya maduka
Ukaguzi hakudhibitisha kuwepo tatizo la katika dai hili kwani nyaraka zinaonesha kutokuwepo tatizo.bali inashauri kuwepo kwa mkanganyiko na wapangaji wake
18.Issue ya deni katika uwanja wa mpira kaitaba.
Uwanja ulikarabatiwa na kiwanda cha sukari kagera kwa madai ya kurejeshewa fedha zake.sehemu ya fedha hazijarudishwa.Tume inapendekeza kufanya muafaka na kiwana au itafute fedha za kulipa deni
19.Kutowajibika ipasavyo kwa ukaguzi wa ndani.
Kipo kwa ajili ya kushauri na kuziba mianya ya matumizi mabaya ya fedha.
Aliyekuwepo amehojiwa juu ya miradi hiyo na kwamba halikuwa hajui lolote na hakuweza kumshauri mkurugenzi ipasavyo
20.Mteuzi katika bodi ya maji.upendeleo kwa mmoja wa madiwani
Waziri mwenye thamana aliteuwa
Hitimisho.
Hatukuweka chumvi,tuliyosema ndiyo ukweli tupu
Namshukuru waziri mkuu kwa kunipa kazi hii ya kukaguzi katika manispaa
Utaratibu wa uwasilisahji wa ripoti maalum tutaipeleka kwa aliyeomba ukaguzi huu.
ASANTENI 
Mwanry anaongea sasa
Kwa niaba ya waziri mkuu naomba nitoa taarifa hii kama ifuatavyo
Maelekezo ya waziri mkuu.
Makosa ya meya anatory kufanya makubaliano bila idhini ya madiwani na taratibu za serikali basi ajipime mwenyewe na kujiuzuru kwa maslahi ya manispaa ya bukoba.
Akikataa basi madiwani wamuondoe
Watumishi wa manispaa wachukuliwe hatua
Bw Khamis kaputa avuliwe madaraka
Mhandisi,mweka hazina nk wapoteze vyeo vyao
Wakandarasi wote waliopata fedha bila taratibu wazirejeshwe.
AMEMALIZA



Alipopewa nafasi, Meya ametangaza kujiuzulu rasmi nafasi yake

Comments

Popular posts from this blog