Mauaji yazidi kutikisa Tarime
Hali ya
usalama Tarime imezidi kutoweka baada ya jambazi lisilofahamika likiwa
na bunduki ambayo haijafahamika aina yake kuendelea kuua watu kwa risasi
hasa wa jinsi ya kiume, ambapo idadi ya waliouawa imefikia saba hadi
sasa na inadaiwa huwaua watu na kupotea bila kutambuliwa.
Jambazi
hilo lisilofahamika liliua watu hao usiku wa Januari 27, mwaka huu
katika maeneo ya Nkende likianza na kumuua Mwendesha Bodaboda, Juma
Marwa Mkazi wa Nkende mjini Tarime akiwa anaelekea nyumbani kwake ambaye
alikufa akiwa hospitali akipatiwa matibabu.
Mganga wa
Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime, Marco Nega alisema tangu
Januari 27 hadi sasa hospitali imeendelea kupokea watu waliouawa na
majeruhi ambao wamefanyiwa uchunguzi na kugundulika wakiwa wamejeruhiwa
kwa risasi katika sehemu mbalimbali za mwili na kwamba watu wapatao 7
wamekwisha kufa mpaka sasa.
“Tumepokea
maiti za watu na majeruhi na tumewafanyia uchunguzi wakagundulika wana
majeraha ya risasi sehemu mbalimbali za mwili, ambapo tayari watu saba
wamekufa wengine wamekufa wakiwa njiani wakienda kwenye matibabu Musoma,
marehemu hadi ni saba,” alisema Nega.
Waliojeruhiwa wakosa huduma ya X-ray
Watu
waliojeruhiwa wameshindwa kupatiwa huduma ya X-Ray kutokana na Hospitali
ya Wilaya kutokuwa na huduma hiyo kwa muda wa zaidi ya miezi 3 na
kusababisha wagonjwa kusafirishwa kwenda Musoma na Mwanza kwa matibabu,
ambapo Samweli Richard amekufa akiwa njiani kuelekea Musoma kwenye
matibabu ikiwamo huduma hiyo ya X-ray.
Hospitali ya Wilaya yashindwa kutoa huduma
Huduma
kwa wagonjwa mbalimbali katika Hospitali ya Wilaya imeshindwa kuendela
vilivyo baada ya kupatwa na misiba miwili ya watumishi wawili, ni baada
ya waume zao kuuawa na jambazi hilo lisilofahamika.
Awali
Januari 26 jambazi hilo lilimuuwa Robert Kisiri (45) mkazi wa Mugabiri
ambapo Mstaafu wa JWTZ Zacharia Mwita(58) na Erick Makanya (25)wote
wakazi wa Kijiji cha Mogabiri Kata ya Kitare Wilayani Tarime walikutwa
wakiwa wameuawa na miili yao ikiwa na majeraha ya risasi mbavuni kushoto
na mgongoni.
Pia
jambazi hilo liliwajeruhi watu watano kwa risasi ambao ni Mgosi Marwa
Mkazi wa Mogabiri, Joseph Richard Mkazi wa Rebu, Gastor Richard Mkazi wa
Rebu, Juma Mwita Mkazi wa Mogabiri na Mkandarasi Binafsi wa ujenzi,
Mwasi Yomami ambao kati ya hao wawili wamefariki wakati wakipatiwa
matibabu.
Kwa
upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya, Justus
Kamugisha amesema wamemkamata mtu mmoja anayeshukiwa kuwa mhusika wa
mauaji ambaye yuko chini ya ulinzi kwa mahojiano na kwamba anazidi
kuongeza vikosi vya doria kuimarisha ulinzi na usalama na kuwasaka
wahalifu.
Wananchi wacharuka
Wananchi
Mjini Tarime waliitaka polisi kuhakikisha jambazi hilo linapatikana
vinginevyo walitaka polisi kuwakabidhi bunduki ili waweze kumsaka
jambazi huyo.
‘Kamanda
kashindwa kazi haiwezekani mtu mmoja aue watu 7 ndani ya siku mbili, huu
ni uzembe wa polisi katika kuimarisha ulinzi, tunaomba tukabidhiwe
bunduki tulisake jambazi,” alisema mwananchi mmoja.
Comments
Post a Comment