KOLETA ADAI HANA MCHUMBA
SWALI
Dada Koleta nakupenda sana hasa nikiangalia kazi zako lakini dada yangu je, unathamini pombe kuwa ni suluhisho la matatizo yako na wewe ni kabila gani? Anna, Dar, 0687005569
KOLETA: Sithamini pombe kuwa ni suluhisho la matatizo ila nakunywa kama watu wengine wanavyokunywa.WANAUME
Koleta eti unajiepushaje na wanaume wakware wanaokutokea kimapenzi wakati ukiwa uswahilini? Salim Liundi, Dar, 0658110395
KOLETA: Mimi ninajitambua na huwa ninakwepa sana vishawishi.
HISTORIA
Dada Koleta nakukubali sana kwa kazi zako nzuri kifupi nataka kujua historia yako. Rama, Tanga, 0656907070
KOLETA: Nimezaliwa Songea nikaanza shule ya msingi mkoani humo ‘theni’ nikahamia Lindi ndipo nilipomalizia elimu yangu ya msingi, sekondari nimesoma Forodhani, Dar mpaka kidato cha nne na baada ya hapo nikajiunga na chuo cha uandishi wa habari lakini sikufanya kazi. Baada ya kumaliza niliingia kwenye mazoezi ya kuigiza.
ANAMPENDA MSANII GANI?
Koleta wewe ni msanii ambaye uko poa sana, mara nyingi huwa napenda ukiigiza muvi zile za hatari kama Misukosuko ila nilikuwa nataka kujua ni msanii gani wa kiume anayefanya Bongo Fleva unampenda? K2, Dar, 0714580516
KOLETA: Filamu za aina zote mimi naweza kucheza nikipata mtu wa kunipa kazi, wasanii wa Bongo Fleva ninawapenda wengi lakini Ali Kiba ni zaidi.
TAFADHALI NIPIGIE
Koleta hongera kwa uigizaji, upo juu, naomba tu uchukue namba yangu unipigie. Tulisoma wote muda mrefu, tafadhali usiache kunipigia. L.G, 0755396203
KOLETA: Sawa nitakutafuta lakini ni vizuri ungeniambia tulisoma wote wapi.
MAFANIKIO
Wewe ni muongozaji mahiri na mtunzi bora wa filamu, vipi kuhusu mafanikio yako? Emmanuel Ntunzwe, Tabora, 0756035421
KOLETA: Sijawahi kutunga hadithi wala kuongoza filamu huwa ninacheza. Kuhusu mafanikio yapo mengi.
TATIZO
Koleta mbona umeadimika sana kwenye gemu? Tatizo ni nini au kiwango kimeshuka? Abuu Sungura, Dar, 0654799098
KOLETA: Ni mihangaiko tu ila nitarudi kwa kasi sana.
USHAURI
Mimi ni shabiki wako, ushauri wangu kwako achana na skendo, anza mwaka 2014 kwa mambo yanayoelimisha jamii. 0654969835
KOLETA: Sina skendo na sipendi. Hata hivyo, asante kwa ushauri wako.
KWA NINI HAOLEWI?
Wewe dada ni mrembo lakini kwa nini huolewi? Mimi pia nimekupenda kama umeridhia nitafute. Martin Kimas, Dar, 0684951599
KOLETA: Kuhusu kuolewa naomba umuulize Mungu, nitakutafuta.
ANAMFAHAMU VIZURI
Koleta mimi nakujua ulikuwa unasoma chuo DSJ (Dar es Salaam School of Journalism) halafu nje kulikuwa na kempu iliyoitwa Manyunyu. Muddy Madiley, 0652672805
KOLETA: Kweli.
UMRI
Koleta una miaka mingapi, elimu gani na je una mchumba? Msomaji, 0765947297
KOLETA: Nina miaka 32, nina diploma ya uandishi wa habari, sina mchumba.
MIPANGO
Kiukweli nakukubali sana dada Koleta uko juu kiutendaji ila vipi una mipango gani hapo baadaye katika filamu? Prosper Mallya, Kilimanjaro, 0757738439
KOLETA: Malengo yangu ni kufanya kazi kwa bidii kwa kutoa filamu zinazoelimisha jamii.
NDUGU
Koleta wewe ni bonge la msanii wa filamu, baadhi ya wasanii wana tabia ya kujisikia na kutojali ndugu zao, je, wewe ni miongoni wao? Mawenje, Dar, 0712474969
KOLETA: Hapana mimi siyo mmoja wao.
Comments
Post a Comment