HABARI MPYAMSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA AKAMATWA NA BANGI JIJINI DAR ES SALAAM
Ferouz (mwenye kofia) akiwa chini ya ulinzi
Kila kukicha kuna wasanii wa maigizo na filamu ambao tunasikia
wamekamatwa na madawa ya kulevya, "unga" katika jitihada za 'kusaka
maisha', wenyewe wanasema kuna ajali kazini. Wasanii hao ambao wengi ni
vijana, na pale wanapoonekana kwenye runinga huwa hamasa kwa wadogo zao
na jamii kwa ujumla, wakipenda kuwa kama wao.
Na mchana
huu, maeneo ya Sinza, kuna taarifa ya mwanamuziki aliyetamba kwenye
muziki wa bongo fleva, Ferouz, sanasana kwa wimbo wake wa Starehe, ambao
ulikuwa ukionyesha madhara ya UKIMWI na virusi vya UKIMWI. Ferouz
anadaiwa kukutwa na bangi, na picha ambazo Gospel Kitaa imezipata eneo
la tukio, zinamuonyesha akisindikizwa na maafande kunako mbele ya vyombo
husika.
Vijana wa
Tanzania tuna shida gani? Kama ni ardhi tunayo, kama ni nguvu tunazo,
sasa nini shida zaidi? Ipo haja ya Operesheni ambazo Askofu Sylvester
Gamanywa ameitisha za Takasika iliyomalizika hivi karibuni, na kisha
kupokelewa na Operesheni Milikisha,
kuwahusisha pia wasanii wa aina zote, maana wanaonekana kukumbwa na
janga hili kwa sana, vinginevyo, vijana ambao ndio nguvukazi ya taifa
watakuwa wakijaa jela za ndani na nje, wakiacha wageni kuja kutawala.
Comments
Post a Comment