BREAKING NEWZZZ: BOTI YA KILIMANJARO 2 YANUSURIKA KUZAMA NUNGWI
- Get link
- X
- Other Apps
Breaking Newss Taarifa
zilizotufikia hivi punde kutoka chanzo chetu cha habari kinasema boti
ya MV Kilimanjaro II mali ya Bharlesa imepigwa na dhoruba maeneo ya
kisiwa cha Nungwi imekosakosa kuzama ikiwa inatoka Pemba kuelekea Unguja
kwa mujibu wa mtoa habari wetu ni kwamba kuna Abiria wengine wameachwa
baharini pamoja na mizigo mingine kutokana na Boti hiyo kupigwa na wimbi
kubwa na kuyumba na kujikuta kuwadondosha abiria pamoja na mizigo
katika bahari kwa sasa boti hiyo inaendelea na safari, mabaharia wa Boti
hiyo wamejitahidi wamewarushia maboya abiria hao ambao inasadikiwa ni
zaidi ya kumi ambao wamewaacha eneo hilo chafu karibu na kisiwa cha
Nungwi eneo ambalo ni chafu sana kwa vipindi mbali mbali katika bahari
ya Hindi, tatizo la ajali hiyo inasadikiwa ni kutokana na upepo mkubwa
uliotokea maeneo hayo na si Boti hiyo kujaza abiria kwa mujibu wa mtoa
habari wetu.
Hapo
juu ni taarifa za uwezo wa abiria wa meli hiyo ambao inaweza kubeba,
taarifa zaidi tutawapa baadae tunaendelea kufuatilia zaidi
ShareThis Copy and Paste
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment