BELINA ALA BONGE 1 LA SUPRISE TOKA KWA KIDUME CHAKE ..... AMZAWADIA ...
Na Imelda Mtema
SIKU chache baada ya kujifungua mtoto wa kike aliyempa jina la Naila, mwanamitindo maarufu Bongo, Belina Mgeni amezawadiwa hereni na cheni vyenye vito vya rubby na mpenzi wake.
SIKU chache baada ya kujifungua mtoto wa kike aliyempa jina la Naila, mwanamitindo maarufu Bongo, Belina Mgeni amezawadiwa hereni na cheni vyenye vito vya rubby na mpenzi wake.
Mtoto wa kike wa Belina aliyempa jina la Naila.
Akichonga na Weekly Exclusive, Belina alisema kuwa furaha yake imeongezeka mara dufu baada ya kupata zawadi hiyo kutoka kwa baba mtoto wake huyo (jina kapuni) ambaye pia hakumsahau na mtoto wao ambaye amepata hereni zenye vito kama yeye.
Mwanamitindo maarufu Bongo, Belina Mgeni.
“Jamani nina raha mpaka basi jamani kwanza kwa kumzaa mwanangu na kingine kwa mume wangu mtarajiwa kunipa zawadi nzuri kama hii, maana imenionyesha ni jinsi gani amefurahia ujio wa mtoto wetu,” alisema mrembo huyo.
Hereni na cheni vyenye vito vya rubby amezawadiwa Belina na mpenzi wake.
Belina na mpenziwe wanaoishi pamoja pande za Mbezi-Beach, wanatarajia kufunga pingu za maisha miezi kadhaa ijayo kushibisha ahadi waliyoiweka tangu walipoanzisha uhusiano.
Comments
Post a Comment