ANGALIA PICHA ZA WAKE ZA WATU, MAKAHABA WANGONOKA NA MADEREVA KWENYE MALORI....HALI INATISHA SANA....!
KILE
kikosi maarufu kilichojizolea sifa kwa utenda kazi wake cha Operesheni
Fichua Maovu (OFM) kilicho ndani ya jumba la Magazeti Pendwa Tanzania,
Global Publishers jijini Dar kinazidi kufichua uovu, twende pamoja ili
kujua.Mwishoni mwa wiki iliyopita, OFM ilitua ‘Mji Kasoro Bahari’
(Morogoro) ambapo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Morogoro, kazi
kubwa ilifanyika.
KAZI YENYEWE
Kazi
ilikuwa kuyafumua madanguro na maeneo ya kujiuzia makahaba ambapo kwa
mujibu wa watoa habari, baadhi ya maeneo mjini humo (hatuyataji kwa
sasa) yamekubuhu kwa biashara ya wanawake kuuza miili yao.
MAENEO YALIYOFIKIWA NA OFM
OFM na jeshi la polisi walijipanga sawa kwa ushirikiano huku wakitumia mbinu za hali ya juu ili kuwanasa machangu hao.
Itigi
Msamvu ni kambi maarufu ya machangudoa hao ambapo wateja wao wakubwa ni
baadhi ya madereva wa magari makubwa ‘malori’ wanaoegesha magari yao
eneo hilo lililopo kandokando ya Barabara Kuu ya Morogoro -Dar es
Salaam.
ILIKUWAJE?
Awali,
wakazi wa eneo hilo walilalamikia uchafuzi wa mazingira na hatari kwa
watoto wao kupata magonjwa ya ajabu kutokana na utupwaji hovyo wa kondom
zilizotumika unaofanywa na machangu hao ambapo watoto hao huziokota na
kuzigeuza maputo.
Wakazi hao walisema kuwa wamesharipoti hali hiyo kwa jeshi la polisi lakini kulionekana kusuasua.
Mbali
na athari za mwanzo, wakazi hao waliwaambia OFM kuwa, kumekuwa na tabia
ya ukabaji na unyang’anyi kwa watu ambao wanakatisha katika vichochoro
vya eneo hilo.
MSIKIE HUYU
“Jamani
OFM tunaomba msaada wenu kwani hapa Msamvu ni jehanam, maasi yote
yanafanyika hapa, ngono mpaka kwenye uvungu wa magari makubwa ambayo
yamepaki, watu wanakabwa, kondom zilizotumika zimezagaa hovyo,” alisema
mkazi mmoja aliyesema anaitwa Mkude.
OFM NA JESHI LA POLISI
Baada
ya kupokea malalamiko hayo, OFM waliwasiliana na jeshi la polisi mkoani
hapo ambapo walisema wapo katika kujipanga kuingiza operesheni ya
kufungua mwaka 2014.
”Ni
kweli kabisa wakazi wa hapo wanapalalamikia sana pale mahali lakini
tumeshajipanga, hata RPC nadhani alishawaambia nyie (OFM) mje mshuhudie
kazi. Tena kama mnaweza, leo si Alhamisi (Januari 9, 2014) kesho Ijumaa
njooni tuingie kazini, sisi hatuna siasa,” alisema afisa mmoja wa
polisi.
SIKU YA TUKIO
Siku
ya tukio ambayo ilikuwa usiku wa saa tano, Ijumaa iliyopita, Kaimu Mkuu
wa Upelelezi wa Wilaya ya Morogoro, Jamal Ibrahim na msaidizi wake wa
karibu, Tausi Mbalamwezi huku OFM wakiwa kwa ukaribu nao, walipafungia
kazi mahali hapo.
Oparesheni
ilifanyika na kufichua maovu mengi, madada poa kibao walidakwa wakiwa
na watu waliojitambulisha kuwa ni madereva wa malori.
Katika
sakata hilo, baadhi ya madereva ambao ndiyo wateja waliingia mitini,
wengine kujifungia kwenye magari yao na kuwaacha machangudoa hao wakiwa
hawana pa kukimbilia na hivyo kunaswa kama ndege kwenye mtego wa mti
wenye ulimbo.
Baadhi ya makahaba walikiri kuliwa uroda na madereva, wakasema ni wateja wao wa siku nyingi na ndipo wanapoponea wao.
“Jamani
tunatubu lakini hao madereva ndiyo wateja wetu wakubwa. Wakija kama hivi
kutoka Dar wanakuwaga na hela sana,” alisema changudoa mmoja bila
kujitaja jina.
HA! HATA WAKE ZA WATU!
Katika
hali ambayo haikutarajiwa, makahaba wawili walidai wao wameolewa lakini
waume zao wapo nje ya mji kikazi ndiyo maana waliamua kujiuza ili
kupata ‘chochote’.
UTETEZI WA MADEREVA
Baadhi
ya madereva waliozungumza na paparazi wetu walikiri kuwa kuna madereva
wenye tabia hiyo ya kuwanunua machangudoa lakini si wote.
“Jamani
kwanza tuwekane sawa, si madereva wote wana tabia ya kununua machangu,
sisi wengine tunajiheshimu sana, hatuwezi,” alisema dereva mmoja
aliyejitambulisha kwa jina la Mafongo baada ya kukutwa pembeni ya lori.
OFM IKAINGIA GESTI
Baada
ya polisi kuwasomba makahaba hao wa kwenye malori, OFM na polisi
wakaenda kuvamia gesti moja inayojulikana kwa jina la Itigi ambapo,
katika hali ya kushangaza, wanawake wawili, mmoja bonge, walinaswa
ndani ya chumba kimoja, kitanda kimoja.
Hawakuwa
na la kujitetea lakini pembeni ya kitanda hicho palikuwa na kondom
kibao. Watoa habari walisema kuwa, wanawake hao wamekuwa wakilala humo
kwa ajili ya kusaka wateja ambao huwaingiza ndani ya chumba hicho
‘kuwahudumia’.
Wanawake hao waliunganishwa na wenzao kwenye gari na kupelekwa kituo kikuu cha polisi cha mjini Morogoro.
Comments
Post a Comment