ANGALIA PICHA VIBAKA WACHOMWA MOTO BAADA YA KUKAMATWA WAKIIBA
Watu
wawili ambao hawajafahamika majina yao wameuwawa kwa kuchomwa moto na
wananchi wanaozaniwa kuwa na hasira kali katika kijiji cha Kagongwa
wilayani Kahama Mkoani Shinyanga baada ya kudaiwa kuiba vitu
mbalimbali ikiwemo Komputa.
Tukio
hilo limetokea leo majira ya saa tano asubuhi baada ya watuhumiwa hao
kujaribu kuwakimbia viongozi wa Sungusungu waliokuwa wanawashikilia
baada ya kuwakamata.
Kwa
mujibu wa Mashuhuda wamesema vijana hao walikuwa ni tishio katika mji
huo kutokana na kuiba marakwamara hivyo wananchi baada ya kuwakamata
wameamua kuwachoma moto kwa madai kuwa iwe ni fundisho kwa
wengine.Wamesema Awali watuhumiwa walikamatwa na sungusungu ya kijiji
cha Iponya wilayani humo Kabla ya kuamriwa wakaoneshe vitu hivyo ndipo
wakapata mwanya wa kukimbia.Diwani wa kata ya Kagongwa Hamis Kashantole
Ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa kata hiyo
amekataa kuzungumzia tukio hilo kwa madai kwamba hana muda wa
kuongea.Jeshi la polisi wilayani Kahama limethibitisha kutoikea kwa
tukio hilo na hadi sasa uchungizi Unaendelea .ANGALIA PICHA ZAIDI
NA MDODOSOAJI
Comments
Post a Comment