ALBINO ATIKISA MIDUME

 Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa! Mwanadada mwenye ulemavu wa ngozi (albino), Fadhila Omary, mkazi wa Mbezi jijini Dar ametikisa midume na kuzua gumzo nchini baada ya kukamatwa mkoani Morogogo kwenye msako wa makahaba.

Albino akiwa mikononi mwa polisi.
KWA NINI?
Unaweza ukajiuliza kwa nini amegeuka gumzo lakini jibu ni kwamba ishu hiyo imemkuta hivi karibuni ikiwa ni miezi michache baada ya Mahakama ya Jiji la Dar ‘Sokoine Drive’ kumuonya kuwa imezichoka kesi zake za kunaswa kwenye misako mbalimbali ya makahaba.

MAMA WA WATOTO WAWILI
Fadhila ambaye ni mama wa watoto wawili, Juni 21, mwaka jana alifikishwa kwa mara ya tatu mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Jiji la Dar ‘Sokoine Drive’, Timothy Lyon baada ya kunaswa kwenye msako wa makahaba.


...Akielekea kituoni baada ya kunaswa katika msako wa makahaba.
HAKIMU MSHANGAO
Baada ya Lyon kumuona alishtuka na kumuuliza ‘hivi wewe Fadhila una matatizo gani? Mimi tangu nihamie mahakama hii kutoka Mahakama ya Wilaya ya Kisarawe, Pwani hapa sijamaliza hata mwaka lakini umeshaletwa mbele yangu mara tatu!’
Hakimu huyo alimweleza hayo Fadhila huku akionesha mshangao mkubwa.

KUMBE MKE WA MTU!
Katika utetezi wake, Fadhila alimtupia zigo la lawama mumewe, aliyezaa naye watoto wawili.
Alisema kuwa mwanaume huyo amekuwa akimpa fedha kiduchu za matumizi hali inayomfanya ajiingize kwenye biashara hiyo.

Baada ya utetezi huo, mumewe alipelekewa barua ya kuitwa mahakamani hapo ambapo alionywa juu ya kuitunza familia yake na mkewe alionywa kutopatikana tena na kesi kama hiyo kisha akapewa ushauri nasaha katika Kitengo cha Ustawi wa Jamii kilichopo mahakamani hapo.
Miongoni mwa mambo waliyoshauriwa ni kubadili mfumo wa maisha kwa  kujitafutia kipato kwa njia nyingine ya halali na kuelezwa madhara ya kuishi kwa kutegemea biashara hiyo haramu.
Baada ya kupewa somo, wote wawili waliahidi kubadilika lakini katika hali ya kushangaza ilidaiwa kuwa Fadhila baada ya kuwapa kisogo maofisa wa ustawi wa jamii, alichofanya ni kuhama mkoa na kwenda kufanyia shughuli hiyo mkoani Morogoro.

OFM KAZINI
Baada ya Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ kupata taarifa hizo ilitoa maelekezo kwenye kitengo chake cha Mtambo wa Kurekebisha Tabia (MKT).
MKT walifunga safari hadi mkoani Morogoro ‘Mji Kasoro Bahari (MKB) na kujiunga na vijana wa Kamanda Faustine Shilogile, Mkuu wa Polisi mkoani humo na kuvamia madanguro na vijiwe mbalimbali vya makahaba.

MKT na vijana wa Shilogile walipata fununu kuwa kuna kundi kubwa la makahaba eneo la Kaumba mjini humo ambapo mmoja wa mapaparazi wa MKT alitangulia eneo hilo kama mteja ndipo Fadhila na wenzake watatu wakamvaa wakitaka kumhudumia.
Wakati wakinadi biashara yao kwa MKT na kuahidi kutoa huduma kwa kadiri anavyopenda mteja (paparazi) ndipo maafande waliokuwa wamejibanza sehemu waliwavamia machangudoa hao na kuwatia nguvuni kwa ajili ya kuwafikisha mbele ya sheria.
Baadhi ya watu waliozungumza na MKT eneo hilo walisema, Fadhila amekuwa tishio kwa kuwapiga bao wenzake kutokana idadi kubwa ya wanaume wanaomgombea huku akiwa na vijana spesho wa kumlinda.

“Huyu dada, hapana chezea kabisa, sijui ana kizizi! Yaani tangu atue hapa Kaumba anawapiga bao wenzake, yaani mpaka aondoke na mteja ndiyo wenzake nyuma wapate wateja. Yaani wanamchukia sijui ana nini,” alisema mmoja wa mashuhuda hao.
Fadhila na wenzake pamoja na wanaume walionaswa wakiwahudumia walitiwa mbaroni na muda wowote watafikishwa mahakamani.

KALAMU YA MHARIRI
Uchunguzi wa OFM uliofanywa katika kila kona ya Tanzania umebaini kuwa hali ni mbaya kwani biashara haramu ya kuuza milii imeshika kasi mithili ya moto wa kifuu. Ni jukumu lako kujilinda kwani kuna hatari ya kukipoteza kizazi hiki kwa Ugonjwa wa Ukimwi.

Imeandaliwa na Richard Bukos, Dar, Issa Mnally na Dustan Shekidele, Morogoro

GPL

Comments

Popular posts from this blog