WOLPER, ZAMARADI NDANI YA BIFU ZITO


Jacqueline Wolper.
Na Shakoor Jongo
STAA wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper amemrushia maneno ya lawama Mtangazaji wa Kipindi cha Take One, Zamaradi Mketema kuwa ni mnafki na adui yake mkubwa katika maisha.


Zamaradi Mketema.
Akizungumza na Amani juzikati, Wolper alisema amegundua kuwa mtangazaji huyo amekuwa akimfuatilia kwa karibu sana maisha yake kwa mtindo wa chanya (negative), akamuomba amuache.
“Nilibadili dini kutoka Ukristo kwenda Uislamu, Zamaradi akanifuatilia, juzijuzi nimerudi kundini (kwenye Ukristo) kwa kusikiliza maneno ya wazazi wangu, akanifuatilia tena.
“Huko nyuma kupitia kipindi chake alikubali nidhalilishwe na waigizaji wenzangu kwa faida yake (hakutaka kufafanua), iliniuma sana. Leo (hivi karibuni)  kaniweka hewani (kwenye redio) bila ya ridhaa yangu. Naomba niseme kuwa naanza kugundua azma yake kwangu ni nini, aniache na maisha yangu,” alilalama Wolper.
Baada ya Wolper kulalamika sana, Amani lilimtafuta Zamaradi kwa njia ya simu ya kiganjani ambapo alisema yeye anawajibika kwa kazi yake hakuna ishu ya kumfuatilia mtu.
“Mimi simfuatilii maisha yake, ni kazi tu. Kama mwandishi wa habari nikipata habari ya mtu natakiwa kubalansi (uwiano) naye,” alisema Zamaradi.

Comments

Popular posts from this blog