TAMBO MPYA ZA NEY WA MITEGO
STAA wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, hivi karibuni alifunguka kuwa hakuna jambo analoepukana nalo kama kukutwa na mchumba wake, Siwema akiwa na mademu wengine maana huwa anazimia.
“Mchumba wangu ananipenda sana na ndiyo maana sasa ninaishi kwa tahadhari kubwa kwani sipendi kumuona Siwema wangu akizimia kwa sababu ya wivu, najitahidi kumlinda kwa kujiepusha kuwa karibu na mademu,” alisema Nay.
Comments
Post a Comment