Serikali yaipongeza UCA-Tanzania kuwanyanyua wasanii chipukizi
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Leah Kihimbi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Baadhi ya wasanii chipukizi wa muziki na sanaa wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na baadhi ya viongozi wa UCA-Tanzania.
Mmoja wa wasanii wa kuchora akionesha kipaji chake cha kuchora michoro anuai kwa jamii kwenye tamasha hilo(P.T)
Picha mbalimbali juu ni baadhi ya wasanii chipukizi wakionesha vipaji vyao kwenye tamasha hilo.
Baadhi ya wasanii chipukizi wakimsikiliza mgeni rasmi kabla ya kuonesha vipaji vyao.
Baadhi ya Wasanii chipukizi mbalimbali waliopata nafasi ya kuonesha vipaji vyao kwenye tamasha hilo.
Mmoja wa wasanii chipukizi akifanya vitu vyake jukwaani.
Na Mwandishi Wetu KATIBU
Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ameipongeza Asasi
ya Ukuzaji Vipaji vya Sanaa na Muziki nchini (UCA-Tanzania) kwa wasanii
chipukizi. Pongezi hizo zimetolewa jana jijini Dar es Salaam na
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Bi. Leah Kihimbi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo. Bi. Kihimbi alisema hayo alipokuwa akizinduwa tamasha la
ukuzaji Vipaji vya Sanaa na Muziki kwa vijana lililoandaliwa na asasi ya
UCA-Tz kwa lengo la kutoa nafasi kwa vijana wenye vipaji kuonesha
vipaji vyao kwa jamii kila mwaka. "...Nimeambiwa kuwa asasi hii
imesajiliwa kwa lengo la kuwashirikisha na kuwaunganisha vijana wenye
vipaji vya sanaa na muziki pamoja na waliokwishafanikiwa katika
kuwezesha kukuza vipaji walivyonavyo," alisema Bi. Kihimbi
akimuwakilisha Katibu Mkuu. "Kimsingi hili ni jambo jema la kusaidiana
na serikali katika kukuza vipaji na kuongeza viwango vya sanaa, ili
kuwawezesha wasanii wetu kukabiliana kikamilifu katika ushindani wa soko
la kimataifa," alisema. "...Nawashauri vijana watumie fursa kama hii
kila kila zinapopatikana katika kufanikisha malengo yao kupitia fani za
sanaa. Kama sote tunavyofahamu kuwa sanaa ni ajira na inanafasi kubwa ya
kubadili maisha ya watu na nchi kiuchumi na kifikra ni vema watu
wakaondokana na dhana potofu kuwa sanaa si kazi ya maana na ni kwa
wasiohitaji kujifunza," alisisitiza. Aidha alitoa changamoto kwa badhi
ya watu kuacha fikra finyu za kuichukulia sanaa kama si kazi kama ilivyo
kazi nyingine, kwani mawazo hayo hayaitendei haki pamoja na kuzingatia
umuhimi wa sanaa kwa jamii. "...Ninapata furaha kubwa kusikia kuwa
tamasha hili litakuwa likifanyika kila mwaka. Ninakupongezeni sana kwa
kubeba sura ya uzalendo unaolenga kuikuza, kuiendeleza na kuipa hadhi
fani ya sanaa na muziki," aliongeza. "...Ninatambua kuwa kazi hii kubwa
na nzuri mnayoifanya ni utakelezaji wa sera ya utamaduni inayosisitiza
na kusimamia maadili ya Mtanzania pamoja na kuzingatia mafunzo na elimu
katika fani zetu. Tunafahamu kuwa utamaduni ni mali ya jamii, hivyo ni
jukumu la wananchi wenyewe kuupenda, kuuthamini na kuuendeleza utamaduni
wetu kwa kutumia kazi za sanaa." Awali akizungumza kabla ya uzinduzi wa
tamasha hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa UCA-Tz, Emmanuel Mushy aliishukuru
Serikali kwa ushirikiano iliouonesha kufanikisha tamasha hilo na kutoa
shukrani kwa makampuni ya Zantel, Coca Cola- Tanzania, Maezeki, LBGY
Media na mtandao wa Thehabari.com kushiriki kuwasaidia vijana
wasiosikika kusikika. Zaidi ya wasanii 25 chipukizi walipata nafasi
kwenye tamasha hilo ya kuonesha uwezo wao kwa jamii wakiwemo baadhi ya
wasanii chipukizi wanaoanza kunufaika na kazi zao kama Menina, M Rap na
Ally Nipishe.
Comments
Post a Comment