RAY C ANATAFUTA BWANA .... HIVI HAPA VIGEZO VYAKE

STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameibuka na kusema kuwa anahitaji mume anayemzidi umri kwa miaka kumi.
Akizungumza hivi karibuni kwenye kituo kimoja maarufu cha runinga, Ray C alisema anahitaji mwanaume mtu mzima anayemzidi miaka kumi, anayejitambua na asiwe mwanamuziki kwani anaamini akiwa na mtu kama huyo uhusiano wao utakuwa mzuri kuliko ule wa awali uliokuwa wa machungu.
“Ninamtaka mwanaume anayenizidi miaka kumi kwani kwa sasa nina miaka 31 japokuwa kwa sasa nafanya kazi kwanza ili nirudi kwenye levo yangu na nitakuwa juu zaidi ya zamani kwa sababu najitambua japokuwa nina hamu sana ya mtoto lakini yote namwachia Mungu.
“Nashukuru sasa hivi niko vizuri nakumbuka  meneja wangu wa kwanza alinikataza nisiwe na uhusiano na mwanamuziki lakini ndiyo hivyo nikajikuta niko na Lord Eyes ambaye alianza kunichanganyia cha Arusha (bangi) bila mimi kujua na kujikuta ninaharibikiwa lakini nimeshamsamehe na ninamuombea heri katika maisha yake,” alisema Ray C.
Aidha, Ray C alisema anamshukuru Mungu kwa sababu hana mume wala mtoto kwa sababu kwa jinsi alivyokuwa mwanzo angejenga picha mbaya sana kwa mwanaye.
“Wakati nilipokuwa na matatizo nilijifunza mengi kwamba hakuna rafiki wa kweli kwa sababu walinipenda nikiwa mzima lakini nilipokuwa naumwa hakuna hata mmoja aliyenipigia simu kunijulia hali zaidi ya mashabiki zangu tu kwa hiyo nimebadilisha mfumo wa maisha yangu,” alisema Ray C.
Miezi kadhaa iliyopita, mwanamuziki huyo alitangaza kuachana na madawa ya kulevya ambayo alikiri kuwa yalimharibia mwenendo mzima wa maisha yake.
JE, UKO TAYARI KOA? VIGEZO NA MASHARTI KUZINGATWA

Comments

Popular posts from this blog