Rais Kikwete awataka wananchi kuwekeza zaidi katika kilimo ili kukuza uchumi wa nchi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete amesema endapo jamii itafanikiwa kuwekeza katika kilimo basi uchumi wa Tanzania utakuwa na kufanikiwa kupiga hatua katika maendeleo ya nchini...
Rais Kikwete ametoa msisitizo huo hii jijini Dar Es Salaam wakati wa mkutano wa saba wa baraza la Taifa la Biashara TNBC uliokutanisha taasisi binafsi na za umma kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi hizo za pande mbili...
Kilimo ni moja ya sekta ambayo imekuwa ikisisitizwa siku hadi siku, ingawa utekelezaji wake umekuwa ukisuasua katika baadhi ya jamii za kitanzania.
Miongoni mwa masuala yaliyozungumzwa katika mkutano huo uliotawaliwa na viongozi kutoka taasisi binafsi na umma ni pamoja na mpango wa Matokeo Makubwa sasa ambao unaonekana kufanikiwa zaidi kutokana na ushirikiano utakaokuwepo baina ya sekta hizo.
Mkutano huo pia umejadili changamoto mbalimbali ikiwemo suala la ajira kwa vijana na namna gani sekta binafsi inaweza kuimarishwa ili iweze kuzalisha ajira.
Viongozi mbalimbali wa serikali na taasisi binafsi akiwemo Waziri Mkuu Mizengo Pinda na mawaziri wa serikali wemehudhuria mkutano huo uliolenga kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi binafsi na za umma.
Comments
Post a Comment