MWANAMUZIKI ALEWA CHAKALI ... AFANYIWA KITU MBAYA
DUNIA kweli haina huruma! Kitendo alichofanyiwa mwanamuziki wa Bendi
ya FM Academia ya jijini Dar anayejulikana kwa jina moja la Flora
alfajiri ya kuamkia Desemba 8, mwaka huu ni kibaya katika jamii ya
Kitanzania.
Flora akiwa amepata kinywaji ili kuchangamsha mwili wake alijikuta
akipigwa na vijana wawili wanaofanya kazi ya kuendesha Bajaj akiwa
amewakodi kwa ajili ya kurudi nyumbani kwake.Tukio hilo lilitokea maeneo ya Mwananyamala jirani na MK Pub jijini jirani kabisa na ofisi ya Msanii Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ limeacha simanzi kubwa kwa wakazi wa eneo hilo.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu inadaiwa kuwa, Flora alipigwa na vijana hao na kuporwa vitu vyake vya thamani ikiwemo simu pamoja na pochi lililokuwa na kiasi cha fedha ambavyo vyote bado havijajulikana thamani yake.
Mbali na kumpiga, vijana hao waliokuwa waliokuwa wakisaidiana kufanya kazi katika Bajaji hiyo wanadaiwa kumvua nguo mwanamuziki huyo ambaye aliwahi kutunga na kuimba kibao cha Sintasahau huku akishiriki kuimba vibao vingine vya FM Academia kama vile Dunia Kigeugeu, Shida na Heshima kwa Wanawake.
“Tulikuwa tumekaa naye hapa tukila chips (MK) baada ya kumaliza kula Flora alionekana akikodi Bajaj ili kurudi nyumbani kwake, baada ya muda tukawaona watu wakikimbilia kule kwenye ofisi ya Chuz, tulipoenda tukamkuta Flora akipewa msaada na mlinzi na mwanamuziki mwingine kutokana na unyama aliofanyiwa,” alisema shuhuda huyo.
Naye mlinzi aliyekutwa eneo la tukio alipoulizwa kuhusina jinsi kitendo hicho kilivyotokea, alisema kuwa aliiona Bajaj ikisimama eneo hilo na watu wanne wakashuka akiwemo Flora na baada ya muda kidogo alimuona mtu akijikokota alipomsogelea ndipo alipomuona mwanamuziki huyo akiwa amevuliwa nguo.
“Wamemfanyia unyama sana wale vijana, sijui nini kingetokea kama ningegundua kabla hawajatenda unyama wao,” alisema mlinzi huyo aliyekataa kutajwa jina lake gazetini.
Flora aliondolewa eneo hilo baada ya kupewa msaada wa nguo na mmoja wa majirani wa eneo hilo ili ajisitiri.
Baada ya tukio hilo, mwandishi wetu alimpigia simu Kiongozi wa FM Academia, Nyoshi El Sadaat lakini hakuweza kupokea ndipo akahamia kwa mwanamuziki wa bendi hiyo, Patcho Mwamba na kumuuliza kama Flora bado yuko FM Academia.
Patcho alikiri uwepo wa Flora katika bendi yao lakini alisema kwamba siku hizi mbilI hajaonekana na alisikitika alipopewa kisanga hicho kilichomkuta.
“Ni kweli tunaye Flora lakini siku hizi mbili hakuwepo kazini dah! Wamemfanyia unyama sana, madereva wengine wa Bajaj si watu wazuri,“ alisema Patcho.
Mpaka sasa haijajulikana kama Flora alitoa taarifa za tukio hilo polisi au la, jitihada za kumtafuta zinaendelea.
GPL
Comments
Post a Comment