MUME NA MKE WAMCHANGIA MTALAKA NA KUMNYOFOA MDOMO RUVUMA.

Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linafanya uchunguzi kuhusu tukio la mume na mke kumshambulia mtalaka wake Faustina Komba (35) mkazi wa jiji la Mbeya kwa kumpiga ngumi, makofi na kumng'ata mdomo wake wa chini na kuuondoa wote. 

Habari zilizopatikana mjini hapa na kuthibitishwa na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Deusdebit Nsimeki zimewataja watuhumiwa hao kuwa ni Hamidu Mapunda na Regina Mpangala  wakazi wa Mshangano, nje kidogo ya Halmashauri  ya manispaa Songea.
Imedaiwa Desemba 7, jioni huko Faustina alishambuliwa kwa kupigwa ngumi, makofi na kung'atwa mdomo wake wa nchini ambao uliondolewa kabisa na Regina ambaye alishirikiana na mume wake Mapunda.
Inadaiwa chanzo cha ugomvi wao Faustina na Mapunda ambaye alikuwa mume wake wa zamani ni kugombea mtoto wao Mussa Mapunda (5).
Imeelezwa kuwa wakati wakigombana mke wake wa sasa (Regina) aliingilia kati akiwa na lengo la kumsaidia mume wake Mapunda.
Kamanda Nsimeki alifafanua zaidi kuwa wakati ugomvi unatokea mke wa sasa wa Mapunda alikuwepo na alishuhudia Mapunda akipigwa kipande cha tofali kichwani ambacho kilisababisha atokwe na damu nyingi, ndipo alipoingilia kati na kuanza kumsaidia mume wake lakini Faustina inadaiwa alimkamata Regina na kumng'ata sehemu ndogo ya mdomo wake wa chini ndipo naye Regina aliamua kumng'ata sehemu ya mdomo wake wa chini na kuundoa wote.
Kamanda Nsimeki alisema kuwa Faustina na Regina wamelazwa katika hospitali ya mkoa Songea kwa matibabu na shauri hilo linasubiri wao wapate nafuu.

Comments

Popular posts from this blog