MKE WA MTU ABAKWA NA KISHA KUNYONGWA

JAMANI jamani! Dunia imefika pabaya zaidi, Mungu asaidie. Mwanamke mkazi wa Chalinze, Mkoa wa Pwani, Moshi Rashid (43) amefanyiwa unyama uliopitiliza na watu wasiojulikana baada ya kumbaka na kumnyonga, inauma sana kwa kweli!
  Mwanamke mkazi wa Chalinze, Mkoa wa Pwani, Moshi Rashid (43) amefanyiwa unyama uliopitiliza na watu wasiojulikana baada ya kumbaka na kumnyonga.
Tukio hilo la kutisha lilijiri usiku wa Desemba 7, mwaka huu Chalinze Kwamwarabu ambapo mwanamke huyo alikwenda kujumuika na ndugu na majirani katika mkesha wa ngoma ya kuwatoa wari siku ya Jumapili.

                                                              Eneo la tukio Chalinze Kwamwarabu.
Mkasa huu unasimuliwa kwa majonzi mazito na mdogo wa marehemu ambaye alikuwa mshehereshaji wa shughuli hiyo ‘MC’, Siwema Rashid.
Alisema: “Mpaka sasa tunashindwa kuelewa kilichotokea maana siku ya tukio tulikuwa naye kwenye ngoma usiku. Alikuwa mchangamfu sana, aliifanya shughuli ipendeze.
“Ilipofika saa nane usiku baadhi ya watu walianza kulala, sasa sijui yeye ilikuwaje mpaka hali hiyo ikamfika maana hao watu walichomfanyia wametuachia historia kubwa sana.
“Walimbaka wakaona haitoshi wakamwingiza chupa ya soda sehemu ya siri ya mbele halafu wakamwingiza chupa ya bia sehemu ya siri ya nyuma.
“Ili kuzidi kutimiza unyama wao, waliondoka na kumwacha kama alivyozaliwa, inauma sana halafu matukio ya hivyo yamekithiri sana.”
Aliongeza: “Marehemu ametuachia jukumu la malezi kwa watoto wake wawili, Sikudhani Juma (18) na Ally Juma (12).”
Naye mtoto mkubwa wa marehemu, Sikudhani akisimulia kifo cha mama yake, alisema: “Nasikitika sikuweza kuuona mwili wa mama hata pale watu walipojazana na kumshangaa.

“Hata polisi na mganga mkuu wa mkoa walipofika kumchomoa zile chupa sikutaka kusogea kabisa, naamini Mungu atawaonesha jambo hao watu hapahapa duniani.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Yurichi Mtei akizungumzia ukatili huo alisema: “Taarifa za tukio hilo bado hazijafika kwangu kutokana na majukumu mengine ya kikazi, isipokuwa nalifanyia kazi kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa.”
Tukio hilo lilifunguliwa jalada kwenye Kituo cha Polisi Chalinze kwa namba CH/RB/3767/2013 MAUAJI.
Mpaka kifo chake, mwanamke huyo alikuwa akiishi na mwanaume mmoja (jina halikupatikana mara moja lakini si aliyezaa naye watoto hao wawili). Alizikwa Jumapili iliyofuata, Chalinze.

Comments

Popular posts from this blog