MKASA MWANAFUNZI D ABAKWA NA KUPEWA MIMBA

Denti huyo akiwa na mwanaye
MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika shule ya Bujingwa, iliyopo Nyakato Mwanza (jina linahifadhiwa), mkazi wa Mabatini jijini Mwanza, alibakwa, kutoroshwa nyumbani kwao na hatimaye kupewa mimba na mtu aliyefahamika kwa jina la Roja (27).
Akizungumza  na mtandao wa GPL hivi karibuni jijini Mwanza akiwa hoi kimaisha baada ya kufukuzwa kwa mwanaume huyo, denti huyo ambaye sasa ana mtoto mwenye umri wa miezi saba, alisema baada ya kutoroshwa kwao, mwanaume huyo alimpa mateso mengi, ikiwa ni pamoja na vipigo vya mara kwa mara.
Mtuhumiwa aitwaye Roja

Akisimulia kwa masikitiko, alidai kuwa Roja alimpa mimba akiwa bado mwanafunzi wa kidato cha tatu mwaka 2012 na kumshawishi atoroke nyumbani kwao ili akaishi naye.
Alidai kuwa, usiku wa Desemba 9 mwaka huu, Roja akiwa na baba, alifika nyumbani na kumtaka aondoke mara moja huku akimtupia virago vyake nje ya nyumba bila kujali kuwa na kitoto kichanga.

Hati ya makubalianao

“Siku hiyo alifika nyumbani na kunitaka niondoke , nilipokataa akaanza kunipiga na chuma kichwani na kunikaba shingoni bila kujali nilikuwa na mtoto mgongoni. Nilipoona hali inazidi kuwa mbaya nikaamua kuondoka zangu na kuja hapa ili nisaidiwe,” alisema mwanafunzi huyo ambaye wakati huo alikuwa katika ofisi za taasisi inayojishughulisha na utetezi wa haki za binadamu iitwayo Farijika.
Katika kuchimba ukweli wa madai hayo, waandishi wetu walizungumza na wazazi wa mwanafunzi  huyo ambao kwa muda tofauti walikiri taarifa za mtoto wao kutoroshwa na kubakwa hadi kuzalishwa na mwanaume huyo.


PF3
Kuhusu manyanyaso anayopata mtoto wao, walisema anastahili matibabu (PF3) ambapo vipimo vilionesha kuwa kweli alifanyiwa vitendo hivyo kwa kuwa alikuwa na majeraha ya ndani kwa ndani.
Baada ya kuthibitisha hilo, Roja aliitwa mbele ya watetea haki hao na kukiri kumnyanyasa mkewe lakini akiahidi kutomnyanyasa tena kabla ya kusaini hati ya makubaliano iliyoshuhudiwa na mashahidi watatu, hati ambayo kama akiivunja atafikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali ikiwemo kubaka na shambulio la mwili.

Comments

Popular posts from this blog