Mangariba 38 matatani Moshi Tanzania
- Get link
- X
- Other Apps
Afisaa
mmoja wa serikali kaskazini mwa Tanzania ameambia BBC kuwa kikundi
kikubwa cha watu waliokamatwa kwa kuhusika na ukeketaji wa wasichana
mjini Moshi watafikishwa mahakamani Jumatano.
Kamishna
wa wilaya katika eneo la Kilimanjaro (Herman Kapufi,) amesema kuwa watu
38 waliokamatwa Jumatatu miongoni mwao ni wazazi wa wasichana waliokuwa
wanakeketwa.
Maafisa
wakuu mjini Moshi Tanzania, waliwakamata wanawake 38 mnamo siku ya
Jumatatu waliopatikana wakiwakeketa wasichana katika eneo hilo.Alisema
kuwa wasichana waliokeketwa wanapokea matibabu.
Haijulikani idadi ya wasichana walioathirika. Lakini ripoti zinasema kuwa walikuwa kati ya umri wa miaka 3 na 16.
Ingawa
ukeketaji ambao umeharamishwa huendelezwa katika sehemu nyingi za Mara
na Dodoma nchini Tanzania , hilo sio jambo la kawaida kutokea mjini
Moshi.
Inaarifiwa
wanawake hao walikamatwa walipokuwa wanacheza dansi ya kitamaduni
wakiwazingira wasichana ambao ndio walikuwa wamekeketwa tu.
Baadhi ya wasichana inaarifiwa bado walikuwa wanavuja damu na wengine wakiwa wanauguza majeraha.
Ukeketaji umeharamishwa nchini Tanzania tangu mwaka 1998 ingawa bado unaendelezwa katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo.
Inakisiwa asilimia 15 ya wasichana pamoja na wanawake wamekeketwa nchini humo
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment