JESHI LA POLISI MKOANI KILIMANARO, LIMEWATIA MBARONI WATU 4 KWA TUHUMA ZA KUSHIRIKI KATIKA MATUKIO MBALI MBALI YA UHALIFU NA UNYANGAJI WAKUTUMIA SILAHA

 Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Koka Moita akionesha Vocha za mitandao mbalimbali walizokutwa nazo watu hao.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Koka Moita akionesha bunduki aina ya Shotgun waliyokutwa nao watu hao.
  Vifaa mbalimbali vya kubomolea.
 Laptop mbili pia zilikuwa ni miongoni mwa vitu walivyokutwa navyo.
 Afisa wa polisi katika ofisi ya kamanda wa polisi akipanga vitu mbalimbali walivyokutwa navyo watu hao wanaotuhimiwa kuwa majambazi.
---
 Na Dixon Busagaga-Globu ya Jamii Moshi 


 JESHI la polisi mkoani Kilimanaro, limewatia mbaroni watu 4 kwa tuhuma za kushiriki katika matukio mbali mbali ya uhalifu na unyangaji wakutumia silaha yaliyotokea mkoani hapa.



Kaimu kamanda wa jeshi hilo, Koka Moita, alisema jeshi hilo lilifanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa hao baada ya kukamata gari lenye namba za usajili T564 AUW aina ya Grand Mark 2 wenye rangi ya siliva, katika maeneo ya Kiusa Manispaa ya Moshi ambalo limesadikika kushiriki kwenye matukio hayo. 



 Alisema dereva wa gari hilo ambaye alifahamika kwa jina la Nicksoni Elias Urio (28) mkaazi wa Majengo Moshi alitoa ushirikiano mkubwa ambao ulipelekea kuwakamata watu 3 ambao wamesadikika kuwa majambazi walioshiriki katika baadhi ya mtukio mkoani hapa. 
  


 “ Baada ya kuwatia mbaroni watumiwa hao, operatini kali ilifanyika yakuwapekuwa na kubaini vitu mbali mbali ikiwemo ikiwemo bumbuki aina ya shotgun ikiwa imekatwa mtutu na kitako cha bunduki hiyo hivyo hatukupata namba zake”alisema na kuendelea kuwa “laptop, 2 aina ya dell na hp, Plate namba 3 na funguo za magari, simu 8 za mkononi , vocha za simu za mitandao yote , ambaye thamani yake haijatulikana, pamoja na vifaa mbali mbali vya kuvunjia”alisema Moita.

 Moita alisema Vocha za simu bado hazijajulikana thamani yake, na uchunguzi unaendelea marautakapokamilisha watuhumiwa watafikshwamahakamani. Aidha Kamanda Moita aliwataka wananch kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kufichua matukio

Comments

Popular posts from this blog