HIVI NDIVYO MWILI WA MWANAFUNZI WA CBE DODOMA MAREHEMU SAMWEL P. KITULA ULIVYO AGWA CHUONI HAPO JUZI
Mnamo
saa nane ( Mchana) mwili wa marehemu Samwel P. Kituliuliwasilishwa chuo
cha CBE Dodoma kuagwa na wanafunzi wenzake. Baada ya hapo mwili huo
unasafirishwa kuelekea mkoani kwao marehemu.
Huu
ni upande wa familia ya marehemu mbele yao kukiwa kuna sanduku
lililohifadhiwa marehemu Samwel P. Kituli, aliyepatwa na umauti tarehe
ya kuamukia December 26,2013 chanzo cha umauti huo ikiwa ni uvimbe wa
Ini kwa mjibu wa Madaktari baada ya vipimo kubainisha tatizo hilo.
Kwaya ya Mtakatifu Cecilia kutoka CBE Roman Catholic iliyoshiriki kwenye kuaga mwili wa marehemu
Watu wakipigwa butwaa kwa msiba huu
Wafanyakazi
wa chuo hiki nyuso zao zikiwa ni zahuzuni kwa sababu ya kipindi kigumu
kilicho jitokeza, ikiwa siku ya leo tena tarehe 27/12/2013 wameondokewa
na mfanya kazi Marehemu Selina Makindi hali ikiwa tete kweli.
eeeeh Mungu tusaidie
Wadau mbali mbali waliohudhulia
Hawa ni viongozi kushoto ni Raisi wa (COBESO) Mhe, Remidius Emmanuelna kulia ni Mshauri wa wanafunzi
Marehemu akinyunyiziwa maji ya baraka kwa ishara ya imani yake aliyebatizwa kwa maji ya baraka
Sala kwa marehemu
Ndugu na jamaa wakiwa na majonzi mazito
Katibu mkuu kiongozi Mhe, Dickson Msigwa kutoka serikali ya wanafunzi akisoma wasifu/historia fupi ya marehemu
Rais wa (COBESO) Mhe, Remidius M. Emmanuel alipopata nafasi ya kusimama na kuzungumza,
''Ilikuwa
tarehe 25/12/2013 nilipopata taarifa ya Bw. Samwel anaumwa nlienda
kumuona lakini nikamkuta mke wake akaniambia amelala basi niliondoka
nakutarajia kesho nirudi tena na marafiki zetu kumuona. Muda wa saa nane
usiku nilipokea simu na kuambiwa Samwel amepoteza maisha.
Samwel alikuwa nitegemeo letu kama serikali akiwa ni mshauri wetu nitamkumbuka Daima''
maneno ya Rais wa (COBESO).
Mshauri
wa wanafunzi Mhe, L. Sikato alipopata nafasi ya kusimama ''Napongeza
serikali iliyopo madarakani kufanya vyema ikiwa nina mwaka wa 7 sijawahi
kuona Serikali ya wanafunzi wanatoa Fedha kwenye mfuko wao na
kuchangia, hizi pongezi ziende kwa Rais wa serikali ya wanafunzi Mhe,
Remidius na timu yake nzima kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa, na huu uwe
mfano mzuri wa kuigwa na serikali itakayo ingia madarakani awamu
nyingine tena''
Chuo kimejitole sanduku la marehemu na kusafirisha mwili huo.
RAMBI RAMBI
Chuo - 200,000/=
Wafanya kazi - 72,000/=
COBESO - 50,000/=
Wanafunzi wote - 173,650/=
Jumla - 495650/=
Muda wa kuaga Rais wa COBESO akitoa heshima za mwisho kwa marehemu
Heshima za mwisho
Safari ya kuelekea
Mshauri wa wanafunzi Mhe, L. Sikato akiwa mstari wa mblele kupeleka mwili wa marehemu Samwel P. Kitula
Ukelewe Mkoani Mwanza.
Ukelewe Mkoani Mwanza.
Comments
Post a Comment