HII NDIO PETE YA KWANZA YA SMARTY IJULIKANAYO KAMA "SMARTY RING" INAYOTUMIA TEKNOLOJIA YA BLUETOOTH KATIKA KUPOKEA SIMU



smarty ring-1

Pamoja na kuwepo Smartwatches sokoni, sasa kuna pete inayoweza kuunganishwa na smartphone na kutoa taarifa (notification) pindi ujumbe, barua pepe, zinapoingia katika simu.



‘Smarty Ring’, ni pete inayounganishwa na smartphone kwa bluetooth, na kumuwezesha mtumiaji ku-control simu yake hata ikiwa mbali na yeye.



Ina buttons zinazoweza kutumika kupokea simu, na kuplay muziki uliopo katika smartphone ya mtumiaji. LED screen ya pete hiyo huwaka pindi mtu aliyeivaa anapopokea e-mail, ujumbe mfupi, facebook na twitter notification, au simu inapoingia, na pete hiyo inaweza pia kutumika kama remote control.



Smarty Ring imebuniwa na engineer Ashok Kumar kutoka Chennai, India.

Pete hiyo imetengenezwa na ‘Bluetooth 4.0 sensor’ inayoweza kuunganishwa na simu yoyote ya Android au iOS kupitia application maalum ya Smarty Ring.

smarty ring-3

Panapokuwa hakuna notification yoyote kwenye simu, LED screen ya pete hiyo inaonesha muda. Simu inapoingia, aliyeivaa pete anauwezo wa kuchagua kupokea au kuikata simu kwa kutumia buttons ambazo ziko pembeni mwa pete hiyo.

smarty ring-2

Smarty Ring zitapatikana kwa gharama ya $275 (442,000 Tshs) pindi zitakapoingia sokoni April mwakani. Mwezi September wabunifu wengine wa Hungary walitambulisha pete kama hiyo ‘Ring Clock’, ambayo yenyewe inaonesha muda pekeyake. SOURCE: MAIL ONLINE

Comments

Popular posts from this blog