DIAMOND ADONDOSHA PATI LA UFUSKA MTUPU .... ONA WATU WALIVYOJIACHIA, VYOMBO NJE NJE

KUFURU ya kufunga mwaka! Dogo anayejua kuzitumia vyema fursa muhimu, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ amefanya yake kwa mara nyingine, safari hii amefanya pati iliyojaa ufuska, Ijumaa linaibumburua. 

Burudani zikitolewa na Kundi la Kibao Kata.
Msanii huyo kwa ‘kolabo’ ya swahiba wake mkuu ndani ya anga la muziki Bongo, Omari Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ alifanya tukio hilo lililoacha watu midomo wazi mwanzoni mwa wiki hii ndani ya Ukumbi wa Business Park uliopo Kijitonyama, Dar.
Pati hiyo ilikuwa ya kumpongeza mtu wake wa karibu katika Wasafi Classic Baby (WCB), Halima Haroun ‘Halima Kimwana’.


Halima Kimwana akionyesha baadhi ya manoti aliyotunzwa.
FUNUNU ZA PATI
Ngoma za masikio ya ‘viranja’ wetu yalinasa fununu za kuwepo kwa kufuru hiyo mapema mwishoni mwa wiki iliyopita na kuanza kuandaa ‘patroo’ maalumu ili kunasa matukio muhimu.

SIKIA FUNUNU ZENYEWE
Akizungumza na waandishi wetu kwa usiri na sauti ya ‘kimbeya’, mmoja wa rafiki wa Diamond (jina kapuni) aliweka wazi kwamba Diamond alipania kumfanyia Halima pati hiyo ikiwa ni moja ya matukio yatakayoendelea kukumbukwa kwa mwaka huu.


Mmoja wa wasanii wa Kundi la Kibao Kata akifanya vitu vyake.
“Diamond amepania kufanya makubwa kwenye sherehe hiyo ya kuzaliwa ya Halima ikiwa ni moja ya matukio yake muhimu yatakayokumbukwa. Itakuwa ni pati ya kufa mtu,” alisema ‘kikulacho’ huyo.
MAANDALIZI
Duru za habari zilizidi kudai kuwa, maandalizi ya sherehe hiyo yaliingiliwa kati na Diamond na kumzuia Halima asitumie fedha zake na kwamba kila kitu na gharama zote za juu zitakuwa juu yake.


Steve Nyerere naye akitoa 'misimbazi' kwa Halima.
SIKIA HII
Katika moja ya maandalizi ya sherehe hiyo, walialikwa wacheza shoo maalumu ‘Kibao Kata’ wakiwemo wake za watu ambao siku hiyo walifanya ‘usodoma’ uliomfanya hata shetani mwenyewe afumbe macho kwa aibu.

SIKU YA SIKU
Hatimaye siku ya sherehe hiyo iliwadia Jumatatu ya wiki hii, mastaa muhimu wa mrembo huyo wakaalikwa. Ngoma ya Kibao Kata na muziki wakalamba 500,000, ikawa ni mwendo wa kumwaga lazi kwa kwenda mbele.


...Mambo ya kumwaga radhi hayo.
MASTAA
Weka mbali Diamond aliyekuwa ‘mwenyeji’ wa sherehe hiyo, wasanii wengine waliodondokewa na bahati ya kuhudhuria pati hiyo iliyotawaliwa na matukio machafu ni pamoja na Nurdin Bilal ‘Shetta’, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Juma Said ‘Chegge Chigunda’, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’, Ommy Dimpoz, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ , Husna Maulid na wengine kibao.


Diamond na Ommy Dimpoz (kulia) wakipata msosi katika 'bethidei' hiyo. Kushoto nyuma ni msanii Shetta.
Katika sherehe hiyo ambayo Halima Kimwana alitimiza miaka kadhaa tangu aanze kuvuta hewa ya oksijeni, muziki wa ladha mbalimbali ulitawala huku nyimbo za ‘kaka mdogo‘ huyo zikichosha ngoma za masikio ya wahudhuriaji.
‘MISIMBAZI’ YATAWALA
Ili neno historia litimie, Diamond alifungua ukurasa wa kumwagia Halima ‘mvua’ ya noti nyingi za shilingi elfu kumikumi zilizokadiriwa kuwa Sh. milioni moja na ushee.


Misimbazi iliyokusanywa katika sherehe hiyo.
Mbali na Diamond, Ommy Dimpoz alijibu mapigo kwa kumimina kiasi kikubwa cha ‘misimbazi’ ambayo ilikaribiana na ile aliyomwaga swahiba yake.
Hata hivyo, wasanii wengine hawakurudi nyuma ambapo walitoa kiasi kikubwa cha fedha na kumfanya Halima kuelemewa na mzigo wa noti nyekundu zilizokaribia shilingi milioni nne.

Burudani zikiwa zimepamba moto.
KISA NA SIRI
Inadaiwa kuwa, kisa cha Diamond kuamua kumfanyia sherehe hiyo Halima, ni moja ya zawadi ya kumtunzia kumbukumbu muhimu za nyimbo zake mpya.


...Huyu akionyesha manjonjo yake juu ya meza.
“Unajua Halima amekuwa akimpa Diamond sapoti kubwa kwenye suala la muziki wake.
“Pia Halima ni mmoja wa memba wa WCB kwa hiyo ilikuwa lazima Diamond kama rais wao amfanyie sherehe ya kufuru,” alisema mmoja wa watu wao wa karibu.


Halima akimlisha keki Chegge.
HALIMA KIMWANA ACHEKELEA
Waandishi wetu walianza kazi yao kwa kumbana Halima azungumzie ishu hiyo ambapo alisema:
“Nilisikia furaha sana na niliamini kweli Diamond  ananipenda na kunithamini. Aliwahi kuniambia kuwa siku yangu ya kuzaliwa atanifanyia pati lakini sikuamini kwani huwa ananitania sana, ikawa sapraizi kwangu.”


Queen Darleen akichukua baadhi ya matukio.
BOFYA HAPA KUMSIKIA DIAMOND
‘Mashushushu’ wetu waliendelea na upekepeke wao ili kujua undani zaidi ambapo Diamond alikiri kufanya hivyo na kuthibitisha madai ya kuwa ilikuwa ni zawadi maalumu.
“Watu wengi hawajui ukaribu wangu na Halima una faida gani, ukweli ni kwamba yule ni zaidi ya dada yangu, tumetoka mbali na amekuwa akinisaidia katika mengi ya kisanii,”alisema.


Halima akipozi na msanii Nay wa Mitego.
KUHUSU UFUSKA
“Jamani, ile ilikuwa sherehe sasa utawazuia watu wasicheze kweli? Ni kawaida kabisa, walikuwa na furaha,” alisema Diamond.

KUTOKA DAWATI LA IJUMAA
Licha ya gazeti hili kumpongeza Diamond na Ommy Dimpoz kwa kuthamini michango ya watu wao wa karibu, linakemea vitendo vya kifuska ambavyo vimekuwa vikifanyika kwenye sherehe mbalimbali za mastaa kwani ni kinyume na utamaduni wetu.

GPL

Comments

Popular posts from this blog