CHENI APANIA KUMUAIBISHA RAY
UAMUZI wa kujitosa kuwania nafasi ya uenyekiti wa kundi la mastaa la Bongo Muvi kwa mwigizaji Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’, umempa wakati mgumu mwenyekiti anayemaliza muda wake wa kuliongoza kundi hilo, Vincent Kigosi ‘Ray’ kwa hofu ya kuidondosha nafasi hiyo tamu.
Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita kwa sharti la kutotajwa jina lake, mmoja wa wasanii wakubwa wa kundi hilo alisema tangu Dk. Cheni atangaze nia ya kuwania nafasi hiyo, Ray amekosa raha kutokana na ubora wa sera ambazo Dk. Cheni amekuwa akizinadi kwa wapiga kura.
Vincent Kigosi ‘Ray’.
“Ni kweli nagombea lakini si kwa ajili ya kumkomoa mtu, kiongozi atachaguliwa kwa kuchuja ubora wa sera zake, hayo wanayosema kuwa nitampindua kutokana na sera zangu, wana haki ya kusema,” alisema Dk. Cheni.
Comments
Post a Comment