ANGALIA PICHA ASKARI WAMPA KIPONDO DEREVA DALADALA

Polisi akimpa kichapo dereva daladala.
WAKAZI  wa  mjini hapa wamekilaani kitendo cha askari wa kituo kikuu cha polisi baada ya kumpa kipondo na kumkwida hadi kumvua nguo hadharani dereva wa daladala aliyefahamika kwa jina la Bello.Tukio hilo lililojaza umati wa watu lililoshuhudiwa na paparazi wetu lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya stendi ya daladala mjini hapa.Mashuhuda wa tukio hilo walisema Bello aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Hiace inayofanya safari zake kati ya Mjini na Mazimbu, alikamatwa kwa kudaiwa kuegesha gari vibaya.
“Stendi ni ndogo Bello aliegesha gari lake akisubiri foleni yake ili apakie, cha ajabu askari akafika na kumpa kibano kabla ya kumsweka ndani,” alisema Wamaga Juma na kuongeza:
Kutokana na kichapo kutoka kwa polisi, nguo za dereva daladala zilivuka.
“Wananchi wenye hasira walitaka kumzingua askari yule, akapiga simu na kuwaita wenzake wa kikosi cha usalama barabarani, walipofika walimbeba Bello na kumpeleka kituoni huku akiwa na kipensi tu.”

Hata hivyo baadhi ya wananchi waliwapongeza askari hao kwa madai kuwa, madereva wengi wamekuwa wakivunja sheria za barabarani hivyo kibano alichopewa Bello kitakuwa fundisho kwa wengine.

Comments

Popular posts from this blog