AJIMWAGIA PETROLI NA KUJIWASHA MOTO MBELE YA KANISA

Mtu huyo mara baada ya kuokolewa na wasamaria.

Mwanaume mmoja amejimwagia petroli na kisha kujilipua moto nje ya Kanisa Kuu la Mt. Petro mjini Vatican mapema jana asubuhi, maofisa walisema.

Sababu za hatua hiyo binafsi bado haijafahamika, isipikuwa tu kwamba mtu huyo ambaye hakutajwa jina alikuwa amebeba kipande cha karatasi chenye namba ya simu ya binti yake.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 51 alikuwa akiungua moto kwenye eneo hilo ndipo padri Myahudi alipokimbilia kwenda kumsaidia kuzima moto huo kwa kutumia jaketi.
Padri huyo baadaye aliungana na maofisa wawili wa polisi ambao walitumia kifaa maalumu cha kukabiliana na moto kuzima moto huo.
Mtu huyo ambaue hakutambuliwa alipatiwa matibabu katika hospitali moja ya jirani na kuhamishiwa kwenye hospitali nyingine kubwa zaidi, akiwa na majeraha makubwa ya moto katika sehemu ya juu ya mwili wake.
Maofisa hao wa polisi walitibiwa katika hospitali hiyo kutokana na kuvuta moshi mzito na majeraha kwenye mikono yao.
Shambulio hilo lilitokea siku moja baada ya Papa Francis kufanya mkutano wake wa mwisho wa mwaka hadharani katika Viwanja vya Mt. Petro.
Mandhari ya Alhamisi asubuhi yalikuwa tulivu yaliyotawaliwa na matukio ya furaha siku moja kabla ambapo maelfu ya watu walikusanyika kumsalimu Papa siku moja baada ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.


Comments

Popular posts from this blog