ZITTO KABWE: SIONDOKI CHADEMA NG'O
- Get link
- X
- Other Apps
Zitto Kabwe akielezea kwa wanahabari kuwa haondoki Chadema kamwe.
Aliyekuwa
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe
amesema haondoki Chadema ng'o. Adai yeye ni mwanachama halali wa chama
hicho, amejiunga na Chadema akiwa na umri wa miaka 16, maisha yake yote
ameyatoa kwa ajili ya kukitumikia chama hivyo hawezi kuondoka Chadema.
Ameyasema
hayo muda huu wakati akiongea na wanahabari katika chumba cha mkutano
kilichopo katika Hoteli ya Serena Posta jijini Dar es Salaam.
Dk. Kitila Mkumbo akiwaeleza wanahabari kuwa Zitto Kabwe hausiki na 'Waraka wa Siri'.
Naye Dk.
Kitila Mkumbo aliyevuliwa ujumbe wa Kamati Kuu Chadema amekubali kuwa
'Waraka wa Siri' uliosomwa kwa wanahabari na Mwanasheria Mkuu wa
Chadema, Tundu Lissu juzi na kusababisha kuwavua vyeo Zitto Kabwe, yeye
na Samson Mwigamba ni yeye aliyeuandaa lakini Zitto Kabwe hausiki
kabisa.
Wakili wa
Zitto Kabwe, Albert Msando ametaja maswali kadhaa ambayo yanahitaji
kujibiwa na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu yakiwemo:
Wakili wa Zitto Kabwe, Albert Msando akitaja maswali mabayo yanahitaji majibu kutoka kwa Tundu Lissu.
-Utaratibu gani uliotumika kuwavua vyeo akina Zitto Kabwe?
-Ushahidi gani alionao au alioutumia kumvua vyeo Zitto Kabwe na wenzake?
-Sababu gani za kumhusisha Zitto Kabwe katika mkakati wa siri wakati Dk. Kitila amesema hausiki?
-Utaratibu gani utatumika kuwaandalia mashitaka?
NA GPL
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment