WOLPER AELEZEA ALIVYOFILISIWA
NYOTA
wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa filamu yake
aliyoitoa kumuenzi marehemu Steven Kanumba iitwayo After Death
ilimlostisha kwa kuwa ilimpatia hasara kubwa.
Alisema hasara aliyoipata na ambayo hata wasanii wenzake huipata inatokana na uwepo wa wasambazaji wachache wa kazi za wasanii, kitu kinachowafanya watu hao kujipangia bei bila kujali gharama ambazo wameingia katika utengenezaji wake.
Jacqueline Wolper.
“Nilitengeneza ile filamu kwa hela nyingi kidogo, kama milioni 35 au
40, nikafanya na uzinduzi pale Leaders Club uliogharimu kama milioni 13
hivi, lakini nilipokwenda kwa Wahindi wakanipa shilingi milioni 25,
yaani inakatisha sana tamaa,” alisema muigizaji huyo wakati alipofanya
mahojiano maalum na waandishi wetu.Alisema hasara aliyoipata na ambayo hata wasanii wenzake huipata inatokana na uwepo wa wasambazaji wachache wa kazi za wasanii, kitu kinachowafanya watu hao kujipangia bei bila kujali gharama ambazo wameingia katika utengenezaji wake.
Comments
Post a Comment