WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII YAENDESHA SEMINA KWA WANAHABARI YA KUJADILI MWENENDO WA MILIPUKO YA MAGONJWA NCHINI


 Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani  (WHO) nchini  Dk. Joyce Saguti (kulia), akitoa  mada kwenye semina hiyo.


Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma wa Wizara hiyo, Saidi Makora (kulia), akifafanua jambo kwenye semina hiyo.


Wana habari wakiwa kwenye semina hiyo











Wapiga picha wakichukua picha katika semina hiyo




Dk. Vida Mmbaga wa Kitengo cha Epideniolojia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (kulia), akitoa mada katika semina hiyo

Wanahabari wakisikiliza kwa makini mada 

zilizokuwa zikitolewa.

Mtalaamu wa Kitengo Epideniolojia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (kulia), Rogath Kishimba akitoa mada katika semina hiyo



Mkuu wa  Kitengo cha Kudhibiti mbu waenezao malaria,  Charles Dismas Mwalimu akitoa mada katika semina hiyo.

Na Dotto Mwaibale

VYOMBO vya habari vimetakiwa kutoa taarifa za milipuko ya magonjwa mbalimbali kwa makini ili kuiepusha jamii kuwa na wasiwasi.

Mwito huo ulitolewa na Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Dk. Joyce Saguti wakati akitoa mada kwenye semina ya wanahabari ya kujadili mwenendo wa milipuko ya magonjwa nchini iliyoandaliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iliyofanyika Dar esSalaam jana.

"Nyinyi wanahabari ni watu muhimu katika kutoa taarifa za magonjwa ya milipuko lakini pia mnapaswa kuwa makini wakati wa utoaji wa taarifa hizo ili kuepusha jamii kuingia katika wasiwasi" alisema Dk.Saguti.

Aliongeza kuwa wanahabri wanatakiwa kuwa mabalozi wa kuandika habari mbalimbali za kujikinga na maradhi katika nchi husika na dunia kwa ujumla.

Alisema kila nchi inapaswa kuwa na uwezo wa kubaini magonjwa mbalimbali ya mlipuko kuanzia ngazi ya chini hadi taifa na kujidhatiti kwa kuunda sera, kuweka kanuni na kuweka fedha.

Alisema jambo lingine ni kujenga maabara za kuthibitisha magonjwa mbalimbali kwa kupewa uwezo kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa na kubaini wageni wanaoingia nchini kuwa hawana magonjwa.

Dk. Saguti alisema maeneo yanayolengwa kuwabaini wagonjwa ni katika viwanja vya ndege, kwenye meli, usafiri wa treni na kwenye mikusanyiko mbalimbali kama michezo ya kombe la dunia na mingine.

"Tangu mwaka 200- 2009 nchi mbalimbali zilitakiwa kujipima kiuwezo ambapo Tanzania ilipojipima iliona bado haijafikia lengo ambapo imeomba muda hadi mwaka 1916 na kila mwaka nchi mwanachama zinatakiwa kutoa taarifa" alisema.

Alisema katika ngazi ya jamii tunataka kuwajengea uwezo wa kugundua magonjwa na katika ngazi ya mikoa kuthibitisha ambapo ngazi ya taifa wanatakiwa kuchukua hatua za kufika eneo husika kuthibitisha na kutoa taarifa Shirika la Afya Duninia (HWO)

Naye Dk. Elibariki Mwakapeche ambaye ni mtaalamu Kitengo cha Epidemiolojia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ameitaka jamii kutoa taarifa mapema pale wanapoona kunadalili la ugonjwa fulani katika maeneo yao ili wahusika waweze kuchukua hatua haraka na kuepusha vifo ambavyo viweza kuepukika.

Dk.Vida Mmbaga alitoa mwito kwa jamii kujenga tabia ya kuwa wasafi hasa mikono ili kuepuka magonjwa ya maambukizi hasa yanayotokana na hewa kama mafua.

"Ni vizuri kwa mtu mwenye kirusi cha mafua na vile vyenye majimaji ni vema wakati akipiga chafya ajivunike mdomo wake kwa kutumia kitambaa na kunawa kwa maji yenye vuguvugu na yale yanayotembea kwani virusi hivyo vinakawaida ya kuishi kwenye unyevunyevu" alisema Dk.Mmbaga.

Comments

Popular posts from this blog