SHIJA ALIZWA NA THEA
SIKU chache baada ya ndoa ya mwigizaji, Ndubagwe Mithayo ‘Thea’ kuvunjika, mwigizaji Deogratius Shija ‘Shija’ ameibuka na kueleza maumivu anayoyapata juu ya tukio hilo.
Akizungumza na Amani hivi karibuni, Shija alisema taarifa za kuvunjika kwa ndoa ya Thea na Mike Sangu zilimuuma na kuwataka vijana wengi kuwa makini kabla ya kuoa na haswa kumshirikisha Mungu kila siku kwenye maombi ili ndoa zao zidumu.
“Ndoa siyo maigizo. Ndoa ni mkataba mkubwa sana ambao wanaingia wanadamu hivyo inapovunjika huwa haileti picha nzuri kwa Mungu, binafsi inaniuma sana,” alisema Shija.
Comments
Post a Comment