MWILI WA MAREHEMU DK.MVUNGI WAPOKELEWA KWA MAJONZI JIJINI DAR ES SALAAM NAKUTOLEWA RATIBA KAMILI YA MAZISHI
- Get link
- X
- Other Apps
Mwili wa
Marehemu Dk. Sengondo Mvungi ukifanyiwa maombi mara baada ya kuwasili
Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Wanachama
wa NCCR-Mageuzi wakiwa wamelibeba sanduku lililohifandhi mwili wa
kiongozi huyo wa NCCR-Mageuzi na Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
Mpya.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akiwa uwanjani hapo.
Baadhi ya waombolezaji waliofika uwanjani hapo.
Mjane wa Marehemu, Bi Anna Mvungi akiwa uwanjani hapo kuupokea mwili wa mumewe
Ndugu wakilia kwa uchungu...
Na Father Kidevu Blog
Mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba mpya na Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Marehemu Dk. Sengondo Mvungi umewasili nchini kutoka Afrika Kusini.
Makumi ya
wakazi wa jiji la Dar es Salaam, ndugu jamaa na marafiki wa Marehemu
dk. Sengondo Mvungi walifika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere
upande wa Mizigo na kuupokea mwili wa kiongozi huyo na mwana familia.
Mapokezi
ya mwili wa Dk. Mvungi aliyefariki juzi kufuatia majeraha ya shambulizi
la majambazi lililomkuta nyumbani kwake nombemba 2 mwaka huu na kupeleka
Nchini Afrika Kusini kwa Matibabu, yaliongozwa na Mkewe mama Anne
Mvungi.
Viongozi
wengine waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba mpya, Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Sinde Warioba, Waziri
wa Uchukuzi, Dk. Sengondo Mvungi, Mwenyekiti wa NCCR-Magezi, na wajumbe
takriban wote wa tume ya mabadiliko ya Katiba mpya.
Sanduku hilo lilifunikwa bendera ya Chama cha NNCR-Magezi. Mwili wa marehemu Dk. Sengondo Mvungi unataraji kuagwa kesho katika viwanja vya Karimjee kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini Kwao Kisangara juu, Wilaya ya mwanga mkoani Kilimanjaro kwa Maziko siku ya jumatatu.
________________
MUDA
|
TUKIO
|
LEO, NOVEMBA 15, 2013 – UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU JK
NYERERE | |
Saa 12:50 jioni
|
Kuwasili kwa
mwili wa Marehemu – Uwanja wa Ndege wa Mwalimu JKN |
KESHO, NOVEMBA 16, 2013 – VIWANJA VYA KARIMJEE
| |
Saa 2:00 – 3:30
asubuhi |
Kuwasili kwa
Wageni, Wananchi na Waombolezaji |
Saa 3:30 asubuhi
|
Kuwasili Mwili
wa Marehemu |
Saa 4:00 – 5:45 asubuhi
|
Ibada ya Misa
Takatifu, Viwanja vya Karimjee |
Saa 5:45 – 6:55
mchana |
Salaam za
Rambirambi na Neno la Shukurani |
Saa 6:55 – 8:40
Mchana |
Kuaga Mwili wa
Marehemu |
Saa 9:00 Alasiri
|
Msafara kupeleka
mwili wa marehemu Kibamba Msakuzi |
KESHO KUTWA, NOVEMBA 17, 2013 – NYUMBANI KWA MAREHEMU
- KIBAMBA, MSAKUZI | |
Saa 2:30 – 4:30
asubuhi |
Ibada ya Misa
nyumbani kwa marehemu |
Saa 5:00 asubuhi
|
Kuanza safari ya
kwenda Chanjale, Kisangara Juu, Mwanga, Kilimanjaro |
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment