Mkesha wa Kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu Sharo Milionea afariki dunia ulivyokuwa ...
Ilikua
ni mwezi november tarehe 26 mwaka 2012 majira ya sa 2 usiku ndipo
ziliposambaa taarifa za kifo cha muigizaji na msanii wa muziki wa kizazi
kipya ‘Bongo Fleva’ Husein Ramadhan Mkieti ‘SHARO MILIONEA’.
Leo tarehe 26 november 2013 familia inafanya kisomo kwa ajili ya
kumkumbuku ya Sharo milionea huku nyumbani kwao Lusanga-Muheza,Tanga.
Jana tarehe 25 november kulikua na mkesha maalum,Mkesha huu
umeambatana na kaswida mbalimbali zinazoimbwa na wanafunzi wa
madrasa,Miongoni mwa watu waliohudhuria kisomo hiki ni pamoja na Kitale
ambae alikua rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea.
Mama mzazi wa sharo milionea katikati ya kitale na rafiki wa kitale
millardayo.com imepiga exclusive interview na mama mzazi wa Sharo
Milionea pamoja Kitale juu ya kazi zilizoachwa na marehemu Sharo
Milionea ikiwemo mikataba mbali mbali na makampuni kama ya Airtel,Azam
pamoja na movie ambazo aliziacha marehemu sharo.
‘Dhumuni la mkesha huu ni kumkumbuka mwanangu,kwa kutaka kumsomea dua
ili mwenyezi Mungu ampunguzie mazito na kumpunguzia madhambi yake,Mpaka
sasa mtandao wa Airtel peke ake ndo walinipatia pesa ambapo walinipa
jumla ya milion 10,lakini wengine kama Azam wao walikuja kutoa rambi
rambi zao nikasikia kule wamefuta mkataba’.
‘Nimefatilia juu ya kiwanja chake kilichokua bunju alichotafutiwa na
mjomba wake,nikamwambia mjomba wake akiuze kwa sababu ya usumbufu maana
mi nipo mbali huku,maana nilikua kila siku nasikia mara wamekichota’.
‘Kuhusu Gari ya Marehemu alikua nayo mudy suma ambaye ni rafiki wa
marehemu kwa hiyo Mudy Suma nilimwambia aliuze lile gari,na kweli Mudy
Suma kaliuza lile gari na pesa akaniletea.
‘Kwa hiyo bado movie tu ndo ninayoijua katika vitu walivyonambia
rafiki zake kuwa marehemu alikua na hiki na hiki ni pamoja na movie kwa
hiyo movie bado ndo sijapata hela,nimeambiwa ni movie moja ambayo
amecheza yeye na kitale na mudy suma’.Mama sharo
Comments
Post a Comment