MASOGANGE ADAKWA

Stori: Gladness Mallya
VIDEO Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ ambaye alipata soo la kukamatwa na malighafi haramu aina ya Ephedrine Julai 5, mwaka huu nchini Afrika Kusini amejaa tele jijini Dar es Salaam, Ijumaa limethibitisha.

Masogange akipozi na Jack Patrick.
Masogange ambaye siku ya tukio alikuwa na nduguye, Melisa Edward baada ya kunaswa na madawa hayo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park jijini Johannesburg nchini humo alihukumiwa kwenda jela miezi 32 au kulipa faini ya shilinghi milioni 4.8 ambapo aliweza kulipa na kuwa huru.
Tangu aachiwe huru, Septemba mwaka huu, msanii huyo akawa hajulikani alipo huku baadhi ya ‘posti’ zake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram zikionesha yupo Tanzania au Afrika Kusini.
Masogange akipozi dukani Bongo.
Jumatatu iliyopita, mida ya saa kumi jioni, paparazi wetu alipigiwa simu na msomaji wa gazeti hili (jina tunalo) akisema amemwona Masogange akiingia kwenye duka la nguo lililopo Sinza Kamanyola, Dar akiwa peke yake.
Paparazi wetu alijipanga kwa kamera na kutia timu kwenye duka hilo ambapo hata hivyo muuzaji alisema aliondoka baada ya kufanya manunuzi ya kawaida.
Jumatano, Masogange alitumbukiza picha kwenye mtandao wake akiwa ndani ya duka hilo na modo maarufu nchini, Jacqueline Patrick.


Jack alipigiwa simu ambapo alikiri kuwa na Masogange siku ya Jumanne kwenye duka hilo. Akasema: “Mimi nilimkuta pale, tukapiga picha tukaachana, basi.”
Kwa kutumia namba yake ya simu ya mkononi, Masogange alipatikana na kukiri yupo Dar lakini akasema hakutaka kuweka wazi kwa sababu anawaogopa sana mapaparazi.

Comments

Popular posts from this blog