Kova amtaja anayeshikilia laptop ya Mvungi
- Get link
- X
- Other Apps
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sulaiman Kova
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sulaiman Kova, amemtaja mkazi
mmoja wa Jiji la Dar es Salaam kwamba ndiye anayeishikilia komputa
mpakato (laptop) ya marehemu Dk. Sengondo Mvungi.
Mtu
huyo (jina tunalihifadhi), mkazi wa Vingunguti, anadaiwa kuwa ndiye
anahodhi ya marehemu aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Kova
alisema jana kuwa jeshi hilo limechukua hatua hizo baada ya kufanya
uchunguzi wa kina katika upelelezi imegundulika kwamba kompyuta ya
marehemu inamilikiwa isivyo halali na mtuhumiwa huyo.
Alisema
mtu huyo ameingia katika sifa ya watu wanaotafutwa bila kificho wanted
person(S) (Sheria hii pia inatumika Kimataifa na kuwa picha ya mtuhumiwa
huyo itaonyeshwa katika vyombo vya habari ili mtu yeyote atakayemwona
na kumtambua ajulishe Jeshi la Polisi kwa madhumini ya kumkamata na
kupata laptop hiyo.
Aliongeza
kuwa, kuna dalili kuwa mtuhumiwa huyo amegundua kwamba anatafutwa
hivyo anakwepa kukamatwa na anajificha maeneo tofauti tofauti ya jiji
ikiwa ni pamoja na kusafiri sehemu mbalimbali nchini kukwepa mkono wa
sheria.
Alisema
Jeshi la Polisi Kanda Maalum linaendea kufanya jitihada kubwa kwa lengo
la kuipata “laptop” hiyo pamoja na simu moja ya marehemu.
Aliwaomba raia wema wasisite kutoa taarifa zitakazosaidia kumkamata mtuhumiwa huyo.
Watuhumiwa kumi walishakamatwa kuhusiana na tukio hilo.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment