IFAHAMU VYEMA BAJAJI INAYOZUNGUKA DUNIA NZIMA
Watanzania wengi tunafahamu Bajaji ni usafiri wa hapa na pale tu, yani sio usafiri wa kubeba abiria kwenye masafa marefu lakini Walimu wawili raia wa Uingereza wamekipiga kibajaji gia na kupita nacho nchi mbalimbali duniani zinazofikia 37.
Ni safari ambayo wameianza August 13 mwaka jana (2012) lakini haijafikia hapa bila matatizo, wanakwambia Bajaji imezingua sana kwenye baadhi ya nchi na kuna wakati injini ilisumbua wakajua ndio mwisho wa safari mpaka wakati mwingine wanalazimika kushuka na kuanza kuivuta wao wenyewe.
Unaambiwa hii rekodi itaingia kwenye kitabu cha Guiness kama watamaliza safari yao ambayo wamepanga kuimalizia Brazil kabla ya December 23 2013 kisha kurudi zao nyumbani Uingereza.
Wanasema wengine wameshindwa kuamini kama wanaizunguka dunia kwa ‘tuktuk’ a.k.a Bajaji ambapo kwenye mpaka wa Kenya na Uganda walisimamishwa na Polisi ambae aliwaambia haamini kuhusu urefu wa safari yao ila kama ni kweli, itakua ngumu wao kupata watoto wa kiume.. labda wa kike.
Comments
Post a Comment