Huyu ndio mrembo wa Kitanzania alietangazwa mshindi wa taji la “Miss Commonwealth Africa” huko London Uingereza.
Mtanzania, Malkia Kassu ( wa tatu toka kushoto) akiwa na washindi wenzake – wote wamevalia taji na kubeba vikombe vya ushindi.
Mashindano ya 2013 yalifanyika London Jumamosi Novemba 26 na kwa mara ya kwanza yalikuwa na mshiriki toka Tanzania.
Malkia Kassu ( jina la kuzaliwa Mulki Kassu Miraj) alichaguliwa malkia wa Tanzania na bara zima la Afrika.
Wateuzi
wa ushindi huo hawakuangalia tu sura, bali tabia, fikra, hamasa na
msimamo wa kimaendeleo wa mhusika ambapo washindani walitoka mataifa
mbalimbali duniani.
“Ninataka
kuiwakilisha nchi yangu na kuwasaidia wenye maisha magumu, niifanye
dunia iwe mahali pazuri zaidi. Nafahamu si kazi rahisi ila nina hakika
kila mmoja wetu akijumuika na mwenzake mabadiliko mema zaidi
yatafanyika. Tanzania ni nchi ya amani na ninaamini amani na mapenzi
vyaweza kuongezeka katika jumuiya zetu.” – Kassu
Kutoka
kushoto ni mdhamini, Ali Sungura, Balozi wa Tanzania Uingereza ,
mheshimiwa Peter Kallaghe, Aisha Mohammed na Afisa Ubalozi Allen
Kuzilwa
Malkia Kassu
Malkia Kassu akipongezwa na marafiki, Andrew Matt na Aisha Mohammed.
Malkia Kassu akiwa na mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva, Diamond karibuni.
Comments
Post a Comment