ATEMBEZWA MITAANI UCHI BAADA YA KUFUMANIWA

Stori: Makongoro Oging’
WANASEMA za mwizi arobaini, ikiongezeka moja mshukuru Mungu! Novemba 16, mwaka huu ilikuwa siku ya aibu kwa bosi Hussein Shaban (35) kufuatia kudaiwa kufumaniwa katika nyumba ya kiongozi mmoja wa Chama cha Mapinduzi (CCM) huko Tegeta jijini Dar es Salaam.

Hussein Shaban akiwa amevuliwa nguo na kupewa kichapo baada ya fumanizi.
Sakata hilo la aina yake lilitokea katika kitongoji cha Nyeishozi, Tegeta kwa kumuhusisha Hussein ambaye ni mfanyabiashara  na mke wa kigogo huyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa.
CHANZO CHA FUMANIZI, KUTOWEKA AMANI
Akisimulia tukio zima mwanzo hadi mwisho, kiongozi huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema miezi miwili iliyopita alianza kuhisi ndani ya ndoa yake kuna jambo lanaloendelea kwa siri baada ya nyumba yake kupoteza amani, mke alibadilika tabia ghafla.

Bwana Hussein akitembezwa mitaani.
“Siku moja nilikuwa natafuta nyaraka za kazini ambazo nilikuwa nimeziweka kwenye begi la kubebea kompyuta mpakato (laptop), lakini sikuzikuta.
“Niligundua vitu vyangu vingi havipo ndani kama vile mashati, suruali, redio ndogo na saa ya ukutani. Nilimuuliza mke wangu akanipa majibu rahisi.

UCHUNGUZI WA KINA WAANZA
“Nilianza uchunguzi, niliwahoji shambaboi wangu kuhusu tabia ya mke wangu ambapo waliniambia kila siku nikitoka kwenda kazini nyuma kuna mtu huingia nyumbani kwangu na kukaa na mke wangu kwa muda mrefu ndani.
“Kwa kidokezo hicho, siku moja nilichukua simu ya mke wangu ya kijanjani, nikaipekua na kugundua namba moja ambayo amekuwa akiwasiliana nayo mara kwa mara. Hii namba aliisevu kwa jina la Mwajuma Jumanne.

...Wananchi wakimpiga picha Hussein aliyefumaniwa na mke wa mtu.
“Ajabu ni kwamba, kwa namba hii nilikuta ujumbe mfupi wa maneno (SMS) wa mapenzi kati ya mke wangu na huyo Mwajuma Jumanne. Nilianza kuhisi kuna jambo.
“Moja ya meseji ilisema yeye (Mwajuma) hana mke! Nikajua huyo Mwajuma ni mwanaume niliyeambiwa na shambaboi kuwa huwa anakuja nyumbani kwangu.

“Pia upelelezi wangu uligundua kuwa mwanaume huyo ama huwa anamuibia vitu mke wangu au alikuwa anapewa.
“Niliwahi kuambiwa kuwa kuna siku mke wangu alimpa mwanaume huyo shilingi elfu sitini (60,000/) na akarudia tena hivi karibuni kumpa kiasi hichohicho,” alisema kiongozi huyo.

Hussein akijikinga sehemu za kichwa wakati akipewa kichapo na wananchi.
POLISI WAPEWA TAARIFA
Alisema kufuatia mambo yote hayo, aliamua kwenda Kituo cha Polisi Wazo, Dar kutoa taarifa ya kupotelewa na vitu akimtaja mwanaume huyo kwamba ndiye anayemtuhumu. Kwa ujasiri mkubwa, kiongozi huyo aliwaambia polisi kwamba mtu huyo angemtafuta mwenyewe, likafunguliwa jalada namba WP/RB//7720/2013 WIZI.

MUME AANDAA SAFARI YA UONGO
Akiendelea kusimulia mkasa huo, kiongozi huyo anasema:
“Siku ya tukio, nilijifanya nasafiri kwenda Dodoma kikazi ili kumpa mwanya mgoni wangu kujitawala, niliondoka nyumbani alfajiri huku nikiwa nimeweka wapelelezi wangu.

“Ilipofika saa tano asubuhi, Hussein aliingia nyumbani kwangu na kuanza kujimwaga kama kwake bila kujua arobaini yake ilikuwa inatimia siku hiyo.
...akizidi kutembezwa mtaani.
FUMANIZI LATIMIA
“Mimi na wapelelezi wangu tulivamia nyumba, tukagonga mlango, mke wangu akafungua. Aliponiona ni mimi alianguka kwa kiwewe.
“Nilichungulia ndani kupitia dirishani nikamwona mgoni wangu akivaa shati. Alitoka mbio kuelekea getini. Nilichomoa bastola na kupiga risasi moja hewani, ikampagawisha, akataka kupanda ukuta.

“Nilipiga filimbi watu wakaja, walipojua kisa, walimvua suruali na kuanza  kumpa kipigo huku wakimtembeza mpaka moja ya sehemu anazofanyia biashara zake za kuchemsha supu na kukaanga chipsi, bahati yake aliokolewa na polisi,” alisema kiongozi huyo.
Alipoulizwa alipo mkewe kwa sasa, alisema: “Nilimtimua mbio, kaondoka zake.”
Hussein akiwa ndani ya gari la polisi waliofika kumnusuru.
KAKA WA MTUHUMIWA
Kaka wa damu wa Hussein aliyejitambulisha kwa jina la Tambwe alisema kitendo alichokifanya mdogo wake ni cha aibu ila anapinga adhabu aliyopewa ya kutembezwa uchi.
“Hili tukio alilofanya mdogo wangu ni baya, hata baba yetu mdogo hapa mjini siwezi kumwambia kwa sababu linaweza kumpa presha,” alisema mtu huyo ambaye alimuwekea dhamana polisi mgoni huyo.

Kaka mwingine wa mtuhumiwa, Hamis alisema mama yao mzazi (hakumtaja jina) na bibi yao waliopo Tabora walizimia baada ya kusikia tukio hilo na wameongea kwa simu na mtendewa ili amsamehe mgoni wake.

MKE WA MTUHUMIWA
Mke wa mtuhumiwa, Pili Muhammed akizungumzia fumanizi la mumewe kwa njia ya simu akiwa Rufiji, Pwani alisema: “Mume wangu si mkweli katika mapenzi yetu tangu siku nyingi ila niliamua kuvumilia nikiamini atabadilika lakini badala yake sasa amekamatwa ugoni.”

Aliongeza: “Siku ya tukio mtoto wetu mchanga alikuwa anaumwa, nilipomuomba mume wangu anisindikize hospitali aliniambia hajisikii vizuri, akabaki nyumbani kulinda nyumba.
“Niliporudi sikumkuta  na mpaka giza linaingia hakurejea, baada ya muda kidogo nikaambiwa amekamatwa ugoni yupo Kituo cha Polisi Tegeta (si Wazo). Ndiyo nikawapigia simu kaka zake wakaenda kumdhamini.”

Comments

Popular posts from this blog