Makamu wa Rais alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa Mwandishi Julius Nyaisanga ( Uncle J )


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah aliewahi kuwa ni mmoja wa viongozi waanzilishi wa Kituo cha Radio One, akitokea Radio Tanzania (RTD).


Marehemu Nyaisangah atakumbukwa sana kwa uwezo wake mkubwa wa kusoma habari pamoja na vipindi vya muziki,Matamshi yake laini na ufasaha mkubwa wa lugha ya Kiswahili, vilimtofautisha kabisa na watangazaji wengine.

Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginard Mengi akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.

Mkuu wa Wilaya ya Bahi,Mh. Betty Mkwasa ambaye alifanya kazi pamoja na Marehemu Julius Nyaisangah akitoa heshima za mwisho.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisaini kitabu cha maombolezo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginard Mengi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Bahi,Mh. Betty Mkwasa.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe pia yupo Viwanjani hapa kushirikiana na Waombolezaji mbali mbali kuaga mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.Kushoto ni Afisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania,Haidan Ricco.

Wadau mbali mbali wapo viwanjani hapa,Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari,Absaloum Kibanda na katikati ni Muimbaji wa Muziki wa Dansi wa siku nyingi,Mzee Hassan Bichuka.


Waombolezaji.

Wasifu wa Marehemu ukisomwa na Bw. Mapunda.

Wanahabari wakichukua tukio zima la Kuaga.




Wadau mbali mbali wakiwemo waliowahi kufanya kazi na Marehemu,wakishiriki msiba huo.

Comments

Popular posts from this blog