Ushiriki wa Jeshi la Tanzania katika Kulinda Amani Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tu

wanajeshi_12fdb.png
Na Lorietha Laurence-Maelezo
JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limetoa taarifa ya maendeleo ya wanajeshi wanaoshiriki kulinda amani kwa nchi mwanachama wa maziwa makuu Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo eneo la Goma.
Taarifa hiyo imetolewa na msemaji wa Jeshi hilo Meja Erick Komba alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.(P.T)
Meja Komba alisema kuwa baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya Kijamii hususan "blogs" kuandika taarifa zisizo rasmi ambazo zinapotosha umma kuhusu ushiriki wa Jeshi la Tanzania katika nchi ya Kongo.
Alieleza kuwa jeshi la Tanzania linashiriki kulinda amani Nchini Kongo kutokana na Rais wa nchi hiyo Mhe.Joseph Kabila kuwasilisha ombi katika kikao cha nchi za maziwa makuu kilichofanyika Julai 12 mwaka jana mjini Addis Ababa, Ethiopia baada ya waasi wa M23 kujitenga na Serikali na kuanzisha mapambano.
"Ushiriki wa Jeshi la Tanzania katika kulinda amani nchini Kongo umetokana na ombi liliwasilishwa na Rais Mhe. Joseph Kabila kwa nchi wanachama wa maziwa makuu ambazo ni Rwanda,Uganda,Tanzania na DRC kusaidia kulinda amani na kuwapokonya waasi wa M23 silaha"alisema Meja Komba .
Meja Komba aliongeza kuwa, jeshi la Tanzania ni sehemu ya SADC Standby brigade iliyotoa mchango wake katika jeshi la Umoja wa Mataifa (MUNUSCO) kinachofanya kazi chini ya "Force Commonder" ambapo majukumu yake makubwa ni kuzuia waasi kujitanua, kuvunja nguvu za waasi na kuwapokonya silaha makundi yote ya waasi.
Naye Msemaji wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bw. Assah aliwaomba waandishi na wadau mbalimbali wa habari kuandika habari zenye uhakika na ambazo hazitapotosha umma.
"Nawaomba waandishi na wadau wa habari tuwe tunatoa taarifa zilizo sahihi ili tusipotoshe umma ukizingatia jeshi letu lipo huko kwa ajili ya kulinda amani na siyo kupigana na M23," alisema Mwambene.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi Kikosi cha Tanzania kiko chini ya MUNUSCO ambao ndio wanaoendesha operasheni ya kulinda amani na Tanzania haipigani na M23 wala haina tatizo na Rwanda kuhusiana na operesheni hiyo.
Pia Rwanda imesaidia Tanzania kwa kuruhusu kikosi kupitisha watu, vifaa na zana kuelekea Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mwisho

Comments

Popular posts from this blog