SAKATA LA MANISPAA YA MOROGORO KUVUNJA KANISA MCHUNGAJI AJA JUU

Sakata  la Halmashauri ya manispaa ya Morogoro  kudaiwa kulivunja kanisa la Winning Faith lililopo kata ya saba saba mkoani hapa,Askofu wa kanisani hilo Dietrich Oswald awasaka vigogo wa Halmashauri hiyo akiwashutumu kulivunja kanisa lake.Haya yamebainishwa na mchungaji kiongozi wa kanisani hilo Josephat Hando .
"Huu ni uonezi uliofanywa na uongozi wa Halmashauri ya manispaa,sisi tumejenga kanisa hilio kwa baraka zote serikali ya mtaa na kata kwa ujumla chaajabu manispaa wamekuja usiku wa manane na kumpora simu mlinzi wetu  Bw Joseph Mtinangi kisha kulivunja kanisani letu na kwamba walipomaliza kazi hiyo walimlejeshea simu mlinzi huyo"alisema Mchungaji.
Mchungaji Alisema"Mimi binafsi pamoja na waumini wangu tulifanya ibada ya na kumshitakia Mungu lakini mwenyekanisa lake Askofu Oswald alikwenda Manispaa kuonana na Meya pamoja na Mkurugezi lakini aliambiwa wako kwenye heka heka za mwenge wiki hii ataendela kuwasatafu"alisema Mchungaji huyo
Mchungaji huyo ameongeza kusema jambo hilo analichukulia kama la uonezi kwani nyumba zilizojengwa usawa na kanisa hilo hazikuvunjwa na badalayake kwenye mtaa mzima kanisa lao pekee ndio lililovunjwa.alipoulizwa watachukua hatua gani zidi ya jambo hilo alilodai la uonezi alisema.
Mtandao huu unaendeleakumtafuta Afisa habari wa  Halmashauri ya manispaa ya Morogoro Bi.Lilian kwa lengo la kusikia kauli ya manispaa kuhusiana na malalamiko ya uongozi wa kanisani hilo,jana mtandao huu ulifika kwenye ofisi ya Afisa huyo na kuelezwa  huko nje ya ofisi kikazi
  Mchungaji kiongozi wa kanisani hilo  Josephat Hando akizunbgumza na mwandishi wa mtandao huu kuhusiana na tukio hilo
 Katika hali ya kushangaza inadaiwa kanisani hilo lilivunjwa kwa sababu liko barabarani huku nyumba iliypo usawa na kanisa hilo ikiachwa kama inavyoonekana Pichani. Kwa sasa uongozi wa kanisani hilo umetia amri ya manispaa na kulisopogeza nyuma kanisa hilo ingawa kwa sasa waumini hao wanasali kwa kujibana kufuati ufinyu wa kanisani hilo..
Na Dustani

Comments

Popular posts from this blog