"Nipo tayari kugombea URAIS endapo wananchi WATANICHAGUA."..Mwigulu Nchemba
Naibu katibu mkuu wa CCM bara, Mh. Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mbunge wa Iramba amefunguka kuwa vurugu zilizotekea bungeni wiki iliyopita zilisababishwa na kambi ya upinzani kukosa akili na kutumia nguvu kubwa ....
Akiongea na mpekuzi wetu , Mwigulu ameitupia lawama kambi ya upinzani na kudai kuwa kambi hiyo imekuwa ikitumia nguvu nyingi badala ya akili na maarifa huku ikisahau kuwa Spika pekee ndo mwamuzi wa mwisho kwa jambo lolote ndani ya bunge....
Mwigulu alienda mbali na kudai kuwa, pamoja na vurugu hizo ambazo zimekuwa zikifanywa na wapinzani kwa lengo la kujiimarisha kisiasa, chama chake bado kina imani kubwa ya kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa 2015 kwa kuwa wapinzani hawana SERA wala UBAVU wa kushindana na CCM zaidi ya makelele na vurugu.
Baada ya Mwigulu kugusia michakato ya uchaguzi mkuu ujao, mpekuzi wetu alitaka kukata kiu yake juu ya tetesi zilizopo kuwa CCM wanamwandaa kugombea URAIS ...
Akijibu swali hilo, Mwigulu ameweka wazi kuwa yeye yupo tayari kuwatumikia wananchi katika nafasi yoyote ile na kwamba wao ndo wenye maamuzi ya mwisho.
"Wananchi ndo waamuzi wa mwisho.Endapo wataona ninafaa kwa Rais, basi ntafanya hivyo kwa sababu nipo tayari kuwatumikia katika nafasi yoyote.
"Najua vijana wengi wananichukia kutokana na chuki zinazopandikizwa katika mitandao ya wapinzani. Ukweli ni kwamba chuki hizo zinatokana na ukweli kwamba mimi ni mtu ninayejua madhaifu mengi ya wapinzani.
"Natoa wito kwa vijana wenzangu kuwapuuza watu hao kwa kuwa hawana nia njema na taifa hili"..Mwigulu
Comments
Post a Comment