KINSHASA MARATHON YAVUNJA REKODI!!


1Mkurugenzi wa Executive Solutions, Aggrey Marealle akizungumza na Waziri wa Michezo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Banza Mukalayi kwenye mbio za Kinshasa Marathon zilizoandaliwa na Executive Solutions. Anayesikiliza ni John Addison, Mkurugenzi wa Wild Frontiers ya Afrika Kusini.2Washiriki wa Kinshasa Marathon wakijiandaa kuanza mbio. Mbio hizo ziliandaliwa na Executive Solutions ya jijini Dar es salaam.3Mkuu wa Alerte Rouge, Fanny Kazadi Nyembwe akimkabidhi zawadi Mutumbe Mande ambaye aliibuka mshindi wa mshindi wa mbio za Kinshasa Marathon. Mbio hizo ziliandaliwa na Executive Solutions ya jijini Dar es salaam.
4Warembo wakiwa wameshikilia mifano ya hundi kwa ajili ya kuwakabidhi washindi wa Kinshasa Marathon. Mbio hizo ziliandaliwa na Executive Solutions ya jijini Dar es salaam.5Mwamvita Makamba, Afisa wa Masuala ya Jamii kutoka Vodacom Afrika Kusini akishiriki mbio za Kinshasa Marathon pamoja na Mdhamini wa Kampuni ya Vodafone ya Uingereza Lord Michael Hastings.6Waandaaji John Addison wa Wild Frontiers, Mwesiga Kyaruzi wa Executive Solutions na Debbie Harrison wakiwa kwenye hafla fupi iliyofanyika baada ya mbio za Kinshasa Marathon kumalizika.
…………..
Na Ibrahim Kyaruzi
Mbio za Kinshasa Marathon zilizofanyika huko Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo wiki hii imepata mafanikio makubwa baada ya kupata washiriki zaidi ya 5,000 idadi ambayo ni kubwa sana kwa marathon ya kwanza.Mbio hiyo iliyodhaminiwa na Vodacom Congo imechangisha kiasi cha shilingi bilioni 1.6 ambazo zitatumika kusaidia watu walioathirika na vita kwenye mji wa Goma uliopo Mashariki mwa nchi hiyo kupitia kampeni ya Alerte Rouge.
Meneja Mradi wa Alerte Rouge wa Vodacom Congo, Fanny Kazadi Nyembwe aliwashukuru waandaaji wa mbio hizo Executive Solutions ya Tanzania, CMCT ya DRC, Wild Frontiers na Deep Blue Media za Afrika Kusini  kwa kufanya kazi kubwa sana kuifanya mbio hiyo ya kwanza jijini Kinshasa kuwa yenye mafanikio makubwa.
“Sisi Vodacom Vongo kupitia kampeni ya Alerte Rouge tumefurahishwa sana na matokeo ya mbio hizi za Kinshasa Marathon kuweza kupata washiriki wengi kuliko matarajio yetu. Executive Solutions pamoja na wadau wengine wametusaidia sana kuifanya mbio hii iwe ya kiwango cha kimataifa na kuweza kuvutia watu wengi ukizingatiia ni mara ya kwanza. Alerte Rouge ni kampeni ambayo inaendeshwa na Vodacom Congo ili kusaidia watu wa Goma ambao kwakweli wameathirika na vita hasa akina mama wajane na watoto yatima. Tayari tumeishapeleka msaada wa chakula na sasa kutokana na fedha hizi tulizopata kwenye mbio hii tutapeleka misaada ya mablanketi, vyandarua, madawa pamoja na kuboresha huduma za afya.” Pia aliwashukuru wakazi wa Kinshasa kwa muitikio mzuri na kujitokeza kwa wingi.
Aggrey Marealle, Mkurugenzi wa Executive Solutions, waandaaji wa mbio hizo alielezea kufurahishwa kwake na mbio hizo na kusema kuwapongeza shirikisho la Riadha la DRC kwa kutoa ushirikiano mkubwa katika masuala ya kiufundi ili kufanikisha mbio hizo.
“Ni mafanikio makubwa sana kwa Kinshasa Marathon kuweza kuwa tukio kubwa la namna hii ukizingatia ni mara ya kwanza jijini hapa. Kilimanjaro Marathon ya kwanza ilipata washiriki 750 lakini Kinshasa Marathon ya kwanza imepata washiriki zaidi ya 5,000 na tumefanya maandalizi katika muda wa mwezi mmoja na nusu muda ambao ni mfupi ukilinganisha na Kilimanjaro Marathon ambapo huwa tunafanya maandalizi kwa muda usiopungua miezi sita.”
Marealle alisema kuwa hii inamaanisha kuwa wananchi wa Kinshasa wameguswa na matatizo yanayowakabili wenzao walioko Goma. na Tutanya mbio nyingine kwenye miji ya Lubumbashi, Kisangani na Goma katika miezi ijayo na tunaamini kuwa watu watazidi kujitokeza hivyo tunawaomba pia Watanzania kujitokeza kwa wingi kushiriki.
Naye Mkurugenzi wa Wild Frontiers Joh Addison aliyaomba makampuni mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati na Afrika nzima kwa ujumla kujitokeza kushiriki katika mbio zijazo ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Vodacom kupitia kampeni ya Alerte Rouge.

Comments

Popular posts from this blog