BALOZI MARMO ASISITIZA USHIRIKIANO KATI YA WATANZANIA WAISHIO CHINA


Balozi akiwa na baadhi ya wahudhuriaji.
Balozi wa zamani wa Tanzania nchini China Mh Philip Marmo ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kupangia Ujerumani, ameagwa rasmi siku ya Jumatano tarehe 26,9,2013 hapa Beijing.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wafanyakazi wa Ubalozi, Watanzania waishio China, viongozi mbalimbali kutoka serikali ya China pamoja na marafiki mbalimbali wa Kichina.


Balozi akiwa na baadhi ya wageni waliohudhuria sherehe hiyo

Balozi Marmo ambaye anatarajia kuondoka leo kuelekea kwenye kituo kipya cha kazi huko Berlin Ujerumani, aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini China mwaka 2012, katika kipindi chake kama Balozi ameweza kunafinikisha mambo mengi, kwa mfano; kuongezeka kwa wawekezaji wa Kichina walioenda kuwekeza Tanzania, kuongezeka kwa miradi ya kimaendeleo kati ya Tanzania na China, kuongezeka kwa watalii wa Kichina walioenda kutalii Tanzania, kuongezeka idadi ya wanafunzi wanaopokea ufadhili wa masomo toka serikali ya china, kuwezesha kuundwa ama kuongeza nguvu kwa jumuiya za Watanzania kwenye miji mbalimbali ya China kama Beijing,Wuhan na Guangzhou huku akiwa mlezi wa jumuiya hizo.

Balozi Marmo pia alishiriki katika vita juu ya madawa ya kulevywa kwa kuwatembelea na kutoa ushauri nasaha kwa wafungwa wa Kitanzania waliofungwa kwenye magereza huko mjini Guangzhou na Hongkong hali iliyopelekea wao kufunguka juu hali halisi ya ushiriki wao kwenye biashara ya madawa ya kulevya kwa kuandika barua zinazoelezea baadhi ya washiriki wa madawa ya kulevya, kwa kufunguka huko kumesaidia kutoa mwanga juu ya halisi na kuwafanya vijana wengi kufahamu uhalisia na adhabu  zitakazowakabiri pindi wakutwapo na madawa hayo, tangu kutoka kwa taarifa hizo, ni wiki kadhaa sasa hakuna Mtanzania aliyekamatwa na madawa ya kulevya nchini China.

 


Balozi Marmo akiwa pamoja na Wageni

Balozi Marmo anawashukuru Watanzania wote kwa ushirikiano walioonesha katika kipindi chote akiwa China, pia amewataka kutoa ushirikiano kwa Balozi mpya ajaye huku akisisitiza ushirikiano kati ya Watanzania na kuwahimiza kuishi kwa kufuata sheria na kanuni. Pia amewataka Watanzania wote waishio China iwe kwa kibiashara, kimasomo au kikazi kujisajili kwenye wavuti ya Ubalozi inayopatika kwenye tovuti ya http://tanzaniaembassy.org.cn/watanzania/jisajili/registers.html kwani kwa kufanya hivyo kutaisaidia ubalozi kuwafikia kiurahisi pindi wapatapo matatizo.
 

Comments

Popular posts from this blog