ANGALIA PICHA ZA KUSHANGAZA ZA NDOA YA JINSIA MOJA KWELI DUNIA IMEKWISHA
- Get link
- X
- Other Apps
Mashoga
na Wasagaji wamefunga ndoa iliyoshuhudiwa na mamia ya watu katika
Kisiwa cha Rhodes Island na Minnesota jana nchini Marekani.
UKISTAAJABU YA MUSA, UTAYAONA YA FIRAUNI…
Ripoti
mbalimbali Agosti Mosi mwaka huu nchini Marekani, zinasema kuwa kwa sasa
nchini Marekani zaidi ya robo ya Wamarekani wanaunga mkono ndoa za
jinsia moja na makanisa mbalimbali yameingia na kuendelea kufungisha
ndoa za aina hiyo.
Usiku wa
kuamkia leo (kwa saa za Afrika Mashariki) katika Jimbo la Minnesota
kumelipuka nderemo na vifijo pale mashoga Zachary Marcus na Gary
McDowell walipobadilisha hati za viapo katika ukumbi wa Jiji wa
Providence (Providence City Hall) mbele ya Meya wa Jiji hilo Angel
Taveras.
McDowell
(28) mtafiti katika Harvard Medical School aliyezaliwa Northern Ireland
na kwa mujibu wa sheria za taifa hizo kwa sasa zinampa haki ya kuweza
kuishi na kuwa na makazi ya kudumu na mumewe.
Marcus
(25) ambaye ni Mwanafunzi wa Brown University akinukuriwa na vyombo vya
habari nchinihumo amesema imekuwa siku ya furaha kwake na ushindi wa
kisiasa.
Majimbo 13 nchini Marekani likiwemo la Wshington ndoa za jinsia maoja zinakubalika bila pingamizi lolote.
Kwa
mujibu wa ripoti iliyotolewa na Kundi la Haki za Mashoga na Wasagaji
imesema 30% ya wakazi waliopo nchini Marekani sasa wanaishi
katika maeneo ambayo ndoa za mashoga na wasagaji ni haki ya msingi.
Watu
akali ya 1,000 hapo jana katika Jiji la Minneapolis (Minnesota)
walikusanyika katika ukumbi wa mikutano wakisherehekea ndoa ya 46 ya
watu wenye jinsi moja ikifungwa na kupewa Baraka zote na Meya R.T.
Rybak.
Gavana wa Jimbo la Minnesota Mark Dayton ametangaza Agosti Mosi kuwa “Freedom to Marry Day” jimbo humo.
Mawakili
wamesema Sherehe za mjini humo, zilikuwa za kufana kutokana na ukweli
kwamba majimbo yaliyo karibu nayo yamekubali ndoa za jinsia moja.
Gavana wa
Chama cha Democrats, Lincoln Chafee ambaye alikuwa kiongozi wa kwanza
kabisa kushabikia ndoa za jinsia moja kisheria, alipokuwa Seneta wa
Chama cha Republican anapanga kuhudhuria kikao cha watunga sheria za
ndoa za jinsia moja.
Pia jana
hiyo hiyo Cathy ten Broeke na Margaret Miles nao wamefunga pingu za
maisha wakiwa ni wasagaji wa kwanza kabisa kufunga ndoa katika
Providence City Hall.
Watunga
sheria waliopo katika Rhode Island chenye waumini wengi wa kikatoliki
wamepigana kufa au kupona kwa miaka 16 sasa hata kupitishwa kwa sheria
za Mashoga na wasagaji.
WAKAZI WA MINNESOTA WAKIUNGA MKONO NDOA ZA JINSIA MOJA AGOSTI MOSI
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment